Fahamu Mambo Muhimu Kabla Hujaanza Kilimo Biashara

Share:

Jambo la kwanza: Hatua kwa hatua za utunzaji wa zao (Farming master-plan)

Katika kilimo biashara, hili ni jambo la kwanza na muhimu sana kulifahamu. Farming master-plan ni muongozo wa shughuri zote unazotakiwa kuzifanya katika kilimo chako tangu kuandaa shamba mpaka kuvuna.
Hii ijumuishe shughuri kama kupanda, kudhibiti magugu, uwekaji wa mbolea na kupulizia madawa ya wadudu na magonjwa. Unatakiwa kujua shughuri hizi zote, muda wa kuzifanya, namna ya kuzifanya na mahitaji yake ili uzifanye. 

Kwa mfano uwekaji wa mbolea: wakati gani uweke? kiasi gani? uwekeje? Unatakiwa ufahamu haya yote kabla hujaanza mradi wako wa kilimo ilii usipate usumbufu wakati wa utekelezaji.

Jambo la pili: Makadirio ya Gharama za Uzalishaji na faida

Hili ni jambo lingine muhimu sana. Naamini unapofanya kilimo biashara hujaamua kulima ili ujifurahishe tu, unalima ili upate faida. Hivyo basi unatakiwa ujue mradi wako utakugharimu kiasi gani katika utekelezaji wake na mwisho wa siku utakulipa kiasi gani? Pengine hutopata gharama halisi lakini ni lazima ufahamuu japo makadirio ya gharama ili kwanza uweze kujipanga lakini pia usikwame katika utekelezaji wa mradi wako.


Kwanini ni muhimu kufahamu mambo haya?
  1. Utajua mahitaji muhimu unayotakiwa kuwa nayo kabla hujauanza mradi wa kilimo 
  2. Utapata fursa ya kuuona mradi wako katika hatua mbalimbali hata kabla hujauanzisha
  3. Utaweza kujua makadirio ya gharama za uzalishaji na faida tarajiwa