Taarifa mbalimbali zinaeleza kuwa ugonjwa huo ulianzia huko nchini Marekani mwaka 1976 na kuingia nchini Kenya mwaka 2011. Aidha, mnamo mwaka 2012 ulianza kuonekana rasmi nchini Tanzania huku ikiathiri maeneo machache na kushamiri kwa kiasi kikubwa katika wilaya ya Babati mkoani Manyara na Simiyu mkoani Shinyanga. Hadi kufikia sasa, ugonjwa huu umebainika kuwepo katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mwanza na Mara.
Chanzo cha ugonjwa
Wataalamu katika tafiti zao wanasema kuwa, ugonjwa huu husababishwa na virusi vya aina mbili vinavyoathiri mmea wa mahindi kwa pamoja ambavyo ni Maize Chlorotic Mottle Virus (MCMV) na Sugarcane Mosaic Virus (SCMV). Virusi hivi husambazwa na wadudu wa aina mbili, ambao ni Thrips pamoja na Aphids, japo kuna wadudu wengine wanaweza kubeba na kusambaza ugonjwa huo kama vile beetles and leafhoppers pamoja na matumizi ya mbegu zilizoathirika.
Mahindi yanavyo athirika
Ugonjwa huu huathiri mahindi katika hatua zake zote za ukuaji. Dalili zikianza kuonekana katika shina la jani hadi kwenye ncha ya jani (changa/ lililokomaa)
Kama ifuatavyo;
Majani
machanga ya juu hugeuka na kuwa na rangi ya njano na hatimaye kukauka
kuanzia pembezoni mwa jani kuelekea katikati na hatimaye mmea kufa.
Mmea
huweza kutoa machipukizi mengi sana.
Mbelewele
hukosa chamvua hivyo mmea kutozaa.
Mahindi
yakishambuliwa wakati yanajaza mbegu, gunzi husinyaa na kuweka mbegu
chache au kutojaza kabisa.
Mahindi
yaliyoathirika hushambuliwa na magonjwa nyemelezi hasa ukungu.
Kwa
mimea iliyoanza kusinyaa, huonyesha dalili za kukomaa kabla ya
wakati, huku hindi likiwa katika hali ya kuchoma maganda na kuonesha
utayari wa kuvunwa.
Aidha,
ugonjwa huo unaposhambulia katika hindi lililokomaa, basi huingia
moja kwa moja katika kiini cha punje.
Madhara
Utafiti uliofanywa na wataalamu mbalimbali wakiwepo wataalamu kutoka Taasisi ya utafiti wa Kilimo ya Seliani (SARI) wamebaini kuwa, sumu hiyo (Aflatoxin) inayotokana na fangasi, husababisha ugonjwa wa saratani ya ini kwa binadamu na wanyama. Utafiti huo pia unaeleza kuwa, ugonjwa huo unaweza usionekane kwa haraka na huweza hata kuchukua muda wa mwaka ndipo kujitokeza. Hivyo basi, ni lazima mataifa yote kuwa makini na kuchukulia jambo hili kwa uzito zaidi.
Utafiti uliofanywa na wataalamu mbalimbali wakiwepo wataalamu kutoka Taasisi ya utafiti wa Kilimo ya Seliani (SARI) wamebaini kuwa, sumu hiyo (Aflatoxin) inayotokana na fangasi, husababisha ugonjwa wa saratani ya ini kwa binadamu na wanyama. Utafiti huo pia unaeleza kuwa, ugonjwa huo unaweza usionekane kwa haraka na huweza hata kuchukua muda wa mwaka ndipo kujitokeza. Hivyo basi, ni lazima mataifa yote kuwa makini na kuchukulia jambo hili kwa uzito zaidi.
Mbinu
za kuepuka ugonjwa huu
Panda
mbegu bora zilizothibitishwa na Taasisi ya Uthibiti wa Ubora wa Mbegu
(TOSCI) nchini.
Usipande
mbegu zilizovunwa msimu uliopita kutoka katika shamba
lililoshambuliwa na ugonjwa.
Safisha
shamba kwa kuondoa magugu na masalia yote ya mazao na
kuyachoma/kuyafukia kuepuka maficho ya wadudu na virusi vya ugonjwa.
Kagua shamba mara kwa mara na kama utaona dalili zilizotajwa hapo
juu, toa taarifa kwa mtaalamu wa kilimo aliye karibu nawe.
Namna
ya kudhibiti
Ng’oa
mapema mahindi yote yaliyoathirika, na kuyateketeza haraka.
Usipande
mahindi katika shamba lililoathirika angalau kwa msimu mmoja. Panda
mazao mengine kama vile viazi mviringo, mihogo kama utakavyoshauriwa
na mtaalamu wa kilimo.
Katika
maeneo yenye ugonjwa, dhibiti wadudu wasambazao ugonjwa huo kwa
kunyunyizia kiuatilifu kulingana na maelekezo ya mtaalamu.
Zingatia
kilimo cha mzunguko wa mazao na toa taarifa mapema kwa afisa ugani wa
kilimo endapo utaona dalili za ugonjwa.
Ugonjwa
wa MLND bado unafanyiwa utafiti kwa undani zaidi na dawa bado
haijapatikana. Hivyo wakulima wote wanatakiwa pindi wanapoona kuna
dalili zozote zimeanza kujitokeza katika mashamba yao, hawana budi
kung’oa mimea yote bila kujali kama mengine hayajaambukizwa kasha
waziteketeze kwa moto.
Hii
ni kutokana na sababu kuwa hata mimea ambayo bado haijaonesha dalili
za kuambukizwa, hana budi kuonesha dalili mapema kwani maambukizi
husambaa kwa kasi sana na kwa muda mfupi.