FAIDA UNAZOWEZA KUPATA KUTOKA KWA NYUKI

Share:

Kufuga nyuki na kuzalisha asali kwa mtindo wa kisasa kwa kujenga nyumba ya nyuki inamwezesha mfugaji kuongeza uzalishaji pamoja na kipato.

Nyumba ya nyuki
Hii ni aina mpya ya ufugaji wa nyuki ambapo unaweza kujenga kibanda au nyumba kisha kuweka mizinga idadi unayohitaji.

Ni kwa nini kujenga nyumba au kibanda?
Ni muhimu kufuga nyuki kwenye kibanda au kwenye nyumba kwa sababu inasaidia kudhibiti wizi wa mizinga, pamoja na wanyama wanaokula asali na kudhuru nyuki.
Inarahisisha utunzaji wa mizinga na kuwafanya nyuki wasihame kwenda sehemu nyingine.
Inasaidia watu wengi kujifunza namna nzuri ya ufugaji wa nyuki, ikiwa ni pamoja na watoto, jambo ambalo linafanya shughuli hii kuwa endelevu.
Ufugaji wa aina hii unasaidia kuwak inga nyuki dhidi ya majanga kama vile moto, na mafuriko.
Inawaepusha nyuki na usumbufu unaoweza kuwafanya wasizalishe kwa kiwango kinachotakiwa.
Uzalishaji unaongezeka. Hii ni kwa sababu mizinga inayotumika ni ile ya kibiashara. Mzinga 1 unapata asali kilo 30 sawa na lita 20.
Chumba cha nyuki Aina ya nyumba
Unaweza kujenga nyumba yenye upana wa futi 3 na urefu wa futi 9. Nyumba hii inaweza kuchukua mizinga hamsini. Halikadhalika, unaweza kujenga kibanda chenye ukubwa sawa na huo.
Eneo linalofaa
Ili kuwa na ufanisi mzuri, nyumba hii inafaa kujengwa nje kidogo ya makazi ya watu.
Kusiwe na mifugo karibu.
Iwe sehemu ambayo watoto hawawezi kufika.
Isiwe karibu na njia ambayo watu wanapita mara kwa mara.
Kusiwe na aina ya mimea ambayo nyuki hawapendi.
Kuwe na maji karibu.

Mavuno
Baada ya kujenga nyumba, kuweka mizinga na nyuki kuingia, unaweza kuvuna kwa mara ya kwanza baada ya miezi mitatu. Utaweza kupata mavuno mazuri endapo utavuna kabla nyuki na wadudu wengine hawajaanza kula asali.
Ni muhimu kuhakikisha kuwa wadudu waharibifu kama vile sisimizi, mende na wengineo wanadhibitiwa ili kutokuathiri uzalishaji wa asali. Hakikisha unavuna kitaalamu ili kuepuka upotevu wa asali. Endapo nyuki wametunzwa vizuri na kwenye mazingira mazuri, unaweza kuvuna asali mara tatu kwa mwaka. Katika mzinga mpya nyuki wana uwezo wa kutengeneza masega kwa siku tatu na kuanza uzalishaji wa asali.