Juisi
ina faida nyingi katika mwili wa binadamu, zipo juisi za aina
mbalimbali ambazo zinatokana na mimea na mizizi aliyoumba Mwenyezi
Mungu.
Juisi ya Tende ni miongoni mwa
juisi zilizojizolea umaarufu mkubwa hasa katika kurekebisha tatizo la
nguvu za kiume.
MAHITAJI
:
- Tende kilo
moja
- Maziwa ya unga au ya ng’ombe lita moja
- Sukari kiasi upendacho.
KUMBUKA : Tende
zina asili ya sukari hivyo hakikisha unaweka kiasi
NAMNA
YA KUTENGENEZA :
- Chukua
tende zako kisha zitoe mbegu zake.
- Hakikisha unatoa mbegu tu na kuziacha tende
kama zilivyo bila kutoa kitu kingine.
- Anza kuzisaga peke yake kwenye brenda
hadi zitakapolainika sawasawa.
- Mimina maziwa yako kidogokidogo kwenye brenda
ili kuzisaga vema jambo litakalosaidia juisi yako kulainika vema.
- Baada ya kutia maziwa yote na kuisaga
sawasawa, tia sukari kiasi upendacho huku ukiendelea kuisaga ili
sukari yako iweze kuchanganyika vizuri na juisi yako.
- Juisi yako itakuwa tayari kwa kunywa sambamba
na kitafunwa chochote ukipendacho kama vile bagia, sambusa, korosho
au karanga.