FAHAMU KUHUSU UMWAGILIAJI WA MATONE (DRIP IRRIGATION SYSTEM)

Share:


UFAHAMU UMWAGILIAJI WA MATONE (DRIP IRRIGATION SYSTEM) : Mfumo wa umwagiliaji wa matone (Drip irrigation system) unafanya kazi kama zile drip za ma hospitalini za kuongezewa maji au damu ambazo huwa tunaziita drip.
Pump – Hii inafanya kazi ya kuvuta maji kutoka kwenye chanzo cha maji na kupeleka shambani moja kwa moja au kwenye tank au sehemu ya kuhifadhia maji (water resevour) kwa kuhifadhi.
Filters/ chujio – Filter zinachuja maji ili takataka na vitu vingine visiingie kwenye mfumo wa umwagiliaji na kuleta shida kama za kuziba pipes na Emmitters ni visehemu vya kutolea maji kwa ajili ya kumwagilia.
Back wash controller/ back flow contorller ni valve zinazozuia maji kurudi nyuma ya mfumo hasa mgandamizo wa maji ( pressure) inapokuwa ndogo. Maji yanatakiwa yawe na uelekeo mmoja tu (Unidirection). Hizi ni kama valves za mishipa ya vein zinavyozuia damu isirudi nyuma.
Pressure regulator au control valve – inafanya kazi ya kudhibiti presha ya maji inayoingia kwenye pipes. Ni muhimu sana kudhibiti pressure maana ikizidi tu unaweza kukuta sio drip tena ila pipes au tape zimepasuka zote.
Water tank/resouvr au chanzo cha maji – kazi ni kusambaza maji kwenye drip, lazima maji yawepo ndio uwe mfumo wa umwagiliaji.
Main line/ pipe – ni bomba kubwa linalotoa maji kwenye tank au kwenye chanzo kingine kwenda shambani kwa ajili ya kusambazwa.
Small poly tubes/tapes hizo ndio zileee zinasambaza maji shambani sasa na ndio zenye vitobo vya kudodondoshea maji.
Kuna connectors pia ambazo zinaunganisha hizo tubes na pipes.
Pia kuna gate valves – hizi zinasaidia kumwagilia shamba kwa awamu, yaani unaweza kumwagilia nusu shamba kwanza ukaendelea na nusu baadae. Gate valves Ikifungwa zinazuia maji kwenda eneo moja na kuruhusu eneo jingine hasa kama maji yana pressure ndogo.
Kuna source ya power kama umeme au solar kwa ajili ya pump lakin pia unaweza kutumia mafuta tu
FAIDA ZA KUTUMIA MFUMO HUU WA UMWAGILIAJI

1.  MATUMIZI MAZURI YA MAJI
Mara nyingi wakulima hawajui kama kumwaga maji hovyo ni tatizo hasa pale yanapopatikana kwa wingi.
Sasa drip inapunguza kupotea maji kwa sababu inadondosha maji kwenye mmea tu.
Kwa wenzangu wa kanda ya kati ambao kuna shida ya maji wataelewa kirahisi au kama unatumia ya DAWASCO yenye mita mtaelewa zaidi

  Kwa sababu mfumo huu unamwagia maji kwenye shina la mche tu, unasaidia sana kupunguza shida ya magugu shambani wakati mmea unapata maji tena ya kutosha magugu yanalala njaa inapunguza usumbufu na gharama za palizi.
Ukimwagia kienyeji kwa sababu unamwaga maji mengi kwa wakat mmoja, maji yanapotea haraka sana na mengine ndio yanaenda kustawisha magugu

3. MATUMIZI MAZURI YA MBOLEA
Kwa mbolea za dukani zinazoyeyuka kwenye maji (water soluble), unaziweka kwenye tank zinayeyuka (kutengeneza solution) na baada ya hapo zinaenda kwenye mimea kwa kupitia matone yanatoka kwenye tubes kumbuka wakati huo magugu yanalala njaa .
Tofauti na kumwaga shimoni ambapo unaweza mwaga lita 5 za maji mbolea inayeyuka na kupotelea pembeni magugu nayo yanasherehekea

4.  HAKI SAWA KWA KILA MMEA
Mfumo wa umwagiliaji wa matone unatoa kiwango sawa sawa cha maji na mbolea kwa mimea yote shambani. Yaani mmea ambao upo karibu na chanzo cha maji unapata kiasi cha maji sawa sawa na mmea ambao upo huko mwisho wa shambani na kwa sababu hii basi mazao yanatoka mengi kwa usawa na kama matikiti mengi yanakua makubwa na yanayokaribiana sana ukubwa.
Tofauti na umwagiliaji wa kawaida ambapo mmea karibu na kisima ndio umapendelewa halafu ile ya mbali inakonda kwa sababu watu wanachoka sana pia kubeba ndoo nenda rudi.

5. INAPUNGUZA GHARAMA YA NGUVUKAZI NA KUPUNGUZA CHANGAMOTO YA NGUVUKAZI
Watu wengi wanaishi mjini wana mashamba vijijini na vijana wanawadanganya sana kuwa wamemwagilia kumbe sio au wamemwagilia kwa kumbe wamerashia tu, utaratibu huu kwa sababu ya kufungua tu na kufunga bomba hata mtoto wa darasa la kwanza anaweza kuelekezwa kufungua na kufunga bomba kama ina kijana wa kazi safi angalau kwa sababu hatumii nguvu kubwa sio rahisi kukudanganya.
Mfumo wa drip unapunguza trembling/ kukanyaga kanyaga shamba ambapo kunasababisha compaction ya shamba na kupunguza circulation ya hewa ardhini.

6.   KUONGEZA UZAAJI
Drip irrigation inaongeza uzaaji zaidi ya mara 3 mpaka 4 dhidi ya mfumo wa kawaida, natumia kwenye matikiti maji, kwa kawaida nilipata tani 4 kwa heka lakini tani 12 kwa drip. Hii inasababishwa na usawa kwenye maji na mbolea.

7.   DRIP ZINAPUNGUZA MMOMONYOKO WA ARDHI.
Tofauti na kumwagilia kienyeji au kwa mitaro, yaani kama unatumia drip na ukaweka matandazo ya plastic (Plastic mulch) umemaliza… hamna palizi… hamna matumizi ya nguvu… mavuno mengi… uzalishaji mkubwa
Pia mfumo wa drip ni mwepesi ambao unaweza kuutumia hata kwenye shamba la kukodi na kuutoa unaweka kwenye kirikuu mpaka nyumbani… kuwe na chanzo kizur cha maji tu

GHARAMA ZA MFUMO HUU
– Mfumo huu ni ghali kidogo hawa kwa wanaoanza kwa sababu roll moja ya mita 2000 inauzwa 1.8M mpka 3.6M za kitanzania ambayo inatosha heka moja tu ya matikiti maji, japo itasaidia sana kuweka mbegu nyingi shambani na kuvuna sana.
Pia utekelezaji wake unahitaji utaalamu kidogo kitu ambacho kinaongeza gharama kwa sababu sio kila mtu anaweza kufunga drip