JIFUNZE NJIA RAHISI YA KUPATA VIFARANGA WENGI WA KUKU

Share:
Kuna njia tofauti za kuanza au kuongeza mtaji kwa mfugaji wa kuku kama vile, kununua kuku wakubwa, vifaranga kutoka kwa wafugaji wengine au kuzalisha vifaranga wako wewe mwenyewe. Kwa wafugaji wengi ambao wana lengo la kufuga kuku wengi wa umri mmoja na kupata mayai mengi au aweze kuuza kuku wengi kwa wakati mmoja wenye umri unaolingana inabidi uwe na vifaranga wengi wa umri mmoja.

Kwa nini muhimu kuwa na vifaranga wengi wa umri mmoja?
Husaidia kupunguza gharama za ufugaji kwa mfano chanjo na tiba.
Husaidia kutunza kuku kitaalam kwa urahisi.
- Husaidia kupata mayai mengi kwa wakati mmoja.
- Husaidia kuuza kuku wengi kwa waakti mmoja.
- Kuwapa uhakika wateja wako

Hivyo kuna njia kuu mbili za upatikanaji wa vifaranga wengi kwa wakati mmoja nazo ni;
- Kwa kuhatamiza kuku wengi kwa wakati mmoja.
- Kwa njia ya mashine ya kuangulia incubator)

Sifa za tetea wa kuhatamia
Kuku mwenye umbo kubwa
Mwenye uwezo na historia nzuri ya kuhatamia na hatimaye kutotoa vifaranga

Sifa za mayai ya kuhatamisha
Mayai ya siku ya mwisho kutagwa ndio yawe ya kwanza kuwekwa yafuatiwe na ya siku zinazofuata

Yasizidi wiki mbili tangu kutagwa
Lisiwe kubwa sana au la duara, • Lisiwe na uvimbe
Yasiwe machafu wala yasiwe na nyufa

Sifa za kiota na chumba cha kuhatamia.
Kuku wanaohatamia watengwe katika chumba ili kuondoa tatizo la kutagiana.
Mlango na dirisha viwekwe wavu ili muda wa mchana mwanga na hewa uweze kuingia ndani.
- Chumba kiwe na nafasi ya kutosha kuweka viota, chakula na maji.
- Ili kutumia eneo vizuri viota vinaweza kutengenezwa ukutani kama mashelfu.
- Viota viundwe vizuri kwa nyasi, maranda makavu ya mbao, au nguo ya pamba lakini isiyo tetroni.

Hatua za kuhatamisha kuku
Kuandaa viota, uchaguzi wa matetea bora na kuandaa mayai.
Tetea wa kwanza akianza kuhatamia muweke mayai yasio na mbegu ama viza.
- Rudia zoezi hili mpaka itakapo fikia idadi ya kuku unao wahitaji.

- Baada ya kupata idadi ya kuku wawekee mayai yenye mbegu.