FAIDA YA JUISI YA UKWAJU

Share:


Tunda la ukwaju ni tunda lenye faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Tunda hili huweza kutumika kutengeneza juisi ambayo matumizi yake yana faida kubwa sana katika afya ya mwili wa mwanadamu.

NAMNA YA KUTENGENEZA JUISI YA UKWAJU. 

Nunua ukwaju wako, ukwaju unapatikana kwa wingi sana masokoni na kwenye supermarkets

- Andaa maji kwenye dishi na uoshe kidogo tuu   baada ya kuuosha chukua ukwaju wako weka kwenye sufuria yenye maji ya saizi na injika jikoni  uache uchemke kwa dakika 10/15 ili uuwe vijidudu 

- Ipua ukwaju wako jikoni na uache kwa muda upoe  andaa maji yako masafi na chujio ili uweze kuchuja juice yako kwa uangalifu zaidi ili upate juice yenyewe 

- Weka sukari kwa kiasi unachopendelea pia ili kupunguza ukali unaweza ukaweka hiliki au vanila ili kupata taste weka juice yako kwenye fridge ili ipoe tayari kwa kunywa.

FAIDA YA JUISI YA UKWAJU. 
Ukwaju chanzo kizuri sana cha antioxidants ambazo zinasaidia kupigana na saratani. 

Ukwaju una carotenes, Vitamini C, flavanoids na vitamin B zote.

Ukwaju unasaidia kupunguza homa na kukupa ulinzi dhidi ya mafua.

kwaju unakuepeusha na ukosefu wa Vitamini C.

Ukwaju unakusaidia kuyeyusha chakula tumboni.

Juisi ya ukwaju hutumika kama kitu cha kustarehesha mwili.

Ukwaju unapunguza cholesterol mwilini.

Ukwaju unasaidia kuwa na moyo wenye afya njema.

Ukwaju ukiunywa unasaidia kupooza koo.

Ukwaju ukiupaka kwenye ngozi unasaidia kutibu uvimbe