KILIMO CHA VIAZI MVIRINGO

Share:


Viazi mviringo au Viazi Ulaya ni zao ambalo lina asili ya zao mzizi )(tuberous crop) na linalodumu, kwa jina la kitalaam linaitwa Solanum tuberosum. Neno “Kiazi” linatokana na maana ya mmea ambao una aina “tuber”yaani chenyewe. Viazi mviringo ni zao muhimu la chakula na biashara katika nchi nyingi zinazoendelea. Viazi hukomaa katika kipindi cha miezi mitatu hadi mitano. Viazi mviringo vina virutubisho vingi mfano vitamin, protin,madini na maji.

ASILI YAKE
Viazi mviringo kwa mara ya kwanza viligundulika huko kusini mwa nchi ya Peru na kufuatiwa kaskazini magharibi mwa nchi ya Bolivia kati ya miaka 8000 na 5000 kabla Yesu hajazaliwa (BC). Na vimekuwa viki sambaa kwa kasi katika maeneo tofauti duniani na kuwa zao la chakula katika nchi nyingi. Hapa Tanzania viazi mviringo kuzalizwa katika maeneo yenye miinuko ya kaskazini kama vile Arusha, Moshi, Lushoto na meneo ya kusini yenye miinuko kama vile Njombe mkoani Iringa na wilaya za mkoa wa Mbeya na mkoa wa Songwe. Pia maeneo ya Morogoro yenye miiunuko hususani Tarafa ya Mgeta yameonekana kuweza kuzalisha zao hili kwa wingi.

AINA ZA VIAZI
Viazi mviringo vipo aina mbalimbali zilizoingizwa Afrika Mashariki kutoka Ulaya ambako huzalishwa kwa wingi.


Aina ya Viazi ni kama zifuatazo
Dutch Robijn – kutoka Holland
inavumilia kidogo ugonjwa wa ukungu
hushambuliwa sana na Mnyauko Bakteria
hupendwa na walaji wengi.
Roslin – kutoka Scotlland
ngozi yake ni nyeupe
ndani ni nyeupe
huvumulia ugonjwa wa ukungu.
Kerr’s Pink
ngozi yake ni nyeupe au nyekundu
ndani ni nyeupe
hushambuliwa sana na ukungu na Mnyauko Bakteria.


Atzimba – kutoka Mexico
huvumilia ugonjwa wa ukungu
Uyole: Kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo uyole kuna aina kama baraka, sasamua, tana, subira(EAI 2329), Bulongwa, kikondo(CIP 720050)

HALI YA HEWA
Viazi Mviringo husitawi vizuri sehemu zenye miinuko kati ya mita 1300 hadi 2700 juu ya usawa wa bahari. Viazi huhitaji mvua za kiasi cha sentimita 25 kwa wiki ambazo hutakiwa kuendela kwa muda wa miezi 3 .5 hii huweza kukuza viazi na kupata mavuno mazuri, pia hutoa mavuno mengi kwenye udongo usio mzina na unaopitisha maji kiurahisi, na uwe na rutuba.

UTAYALISHAJI WA SHAMBA
Shamba linatakiwa kuandaliwa vituta vidogo vidogo kwa nafasi ya sentimita 75 kutoka tuta hadi tuta, hii husaidia kuhifadhi udongo na maji na hutoa nafasi nzuri wakati wa upanukaji wa viazi. Inashauriwa pia kama matuta hayajatumika basi ni muhimu kujaza udongo kwenye shina kwani pingili za chini kwenye shina ni lazima zifunikwe na udongo ili zitoe viazi kwa wingi na hivyo mavuno huongezeka

UTAYALISHAJI WA MBEGU
Tumia viazi vyenye umbile dogo kama mbegu, hutakiwa kuwa na upana wa yai au upana wa sentimita 3 – 6. Kiasi cha robo tatu za tani huhitajika kuotesha ekari 1 sawa na tani 1.85 kwa hekta 1. Mbegu hazitakiwi kuhifadhiwa kwenye giza nene kwani zitaanza kutoa vichipukizi virefu vyeupe.

SIFA ZA MBEGU BORA ZA VIAZI
Zenye kutoa mazao mengi zaidi kutoka kwenye shina moja
ziwe zimechipua vizuri na ziwe na machipukizi mengi zaidi ya manne
zisiwe na wadudu pamoja na magonjwa
zitoke katika aina ambayo haishambuliwi na magonjwa kama vile ukungu na mnyauko
zenye ukubwa wa wastani unaolingana na ukubwa wa yai la kuku

UPANDAJI
Viazi hupandwa kipindi mvua zinapotaka kuanza, kuchelewa kuotesha kutapunguza kipindi cha ukuaji wa ile mizizi ili iwe viazi na hivyo kukabiliwa na kipindi cha ukavu. Uoteshaji hufanyika kwa mikono na mbegu ziwekwe chini udongo kwa kina cha sentimita 10. Kama mbegu zitaoteshwa bila matuta basi zioteshwe kwa kina cha sentimita 15 na kufunikwa na udongo mchache na wakati wa palizi udongo utaongezwa ili kuongeza utoaji wa viazi kwa wingi. Nafasi ya kuotesha ni sentimita 75 toka mstari hadi mstari na sentimita 23 – 30kwa mche hadi mche.

MBOLEA
Mbolea ya asili (samadi au mboji) ni vema kutumia ili uweze kupata viazi vingi katika shamba lako.

UPALILIAJI & UNYEVU
Zao la viazi likioteshwa kwa nafasi zilizoshauriwa basi huweza kufunika ardhi yote na hivyo kugandamiza magugu, hii husaidia kwa kipindi cha wiki 6 za mwanzo. Katika mpando wa matuta, basi huwa ni kuondoa magugu na kujaza udongo kwenye mashina.Palilia viazi wiki mbili au tatu baada ya kuchomoza. inulia udongo kufanya tuta zuri ili pawepo na unyevu wa kutosha na kufunika viazi kutokana na mwanga wa jua.

WADUDU
Nondo wa viazi:
Wadudu huathiri viazi vilivyooteshwa wakati ambao sio wa msimu wa viazi. Viwavi wanaoanguliwa huingia ndani ya viazi na kusababisha kuoza. Pia huingia ndani ya viazi wakati vikiwa stoo.
Kuzuia:– Otesha viazi katika kinachoshauriwa au zaidi ya sentimita 3 kwani kiwavi aingiae ndani ya hawezi kuchimba kina kirefu na inulia matuta wakati viazi vinakuwa, hii husaidia kuzuia nondo kutaga mayai.

Minyoofundoo:-Hushambulia viazi vilivyoachwa kwa muda mrefu ardhini na kwenye ardhi iliyoathirika na mmomonyoko.
Kuzuia:
– Usioteshe mbegu ambazo zimeshambuliwa na wadudu.
– Andaa shamba mapema ili masalia yote ya mazao yaweze kuoza ili kutoruhusu makazi ya minyoo fundo.

UVUNAJI
Viazi huwa tayari kuvunwa baada ya miezi 3 hadi 5 kutoka kupanda. mda wa kuvuna unategemea na mda wa kupanda na dhumuni la zao. Uvunaji wa viazi hufanyika kwa kutumia jembe la mkono, viazi vikishang’olewa kutoka chini ya udongo visiachwe kwa muda mrefu kwani vitabadilika rangi na kuwa kijani.
Ili kuifanya ngozi ya viazi kuwa ngumu na isiharibike kirahisi basi mashina yote yanyofolewe wiki 2 – 3 kabla ya kuvuta viazi juu ya udongo. Baada ya viazi kuvunwa haviwezi kuhifadhiwa kwa muda mrefu kwani huanza kuchipua. Viazi huweza kuhifadhiwa kwenye ardhi, lakini si zaidi ya wiki 6 kwani vitakabiliwa na magonjwa na kushambuliwa na minyoo fundo. Kuvitunza viazi ardhini utahitajika kuvifunikia na nyasi ili visibadili rangi ya ngozi kwa kupigwa na jua, usiache viazi shambani bila kufunika kwa nyasi au udongo kwa mda mrefu.


UHIFADHI
Viazi vya chakula viiafadhiwe kwenye ghara hewa ya kutosha pasiwe na unyevunyevu na joto kali, Viazi vilivyowekwa ghalani visilundikwe kwa kina kirefu, visambazwe ili visipate joto.