MATAYARISHO NA UENDESHAJI WA KITALU CHA MBOGA
Kitalu ni nini?
Kitalu
ni mahali ambapo miche huoteshwa na kutunzwa kabla ya kupandikizwa
Kwenye bustani au shambani Kwenye mashimo. Mavuno mazuri ya kilimo
cha mboga na matunda utategemea sana matunzo bora ya miche kuanzia
hatua ya kitalu kwa sababu kitalu ni sehemu mama katika uzalishaji wa
miche. Mkulima anapaswa awe mwangalifu katika kuchagua mahali pazuri
pa kuweka kitalu. Pamoja na kuwa mwangalifu katika kuchagua eneo
linalofaa vile vile mkulima afahamu mbinu za kutayarisha na kutunza
miche Kwenye kitalu.
Kuchagua eneo la kitalu
Mambo
Muhimu ya Kuzingatia
-
Eneo
la kitalu lisiwe na magugu sugu kama vile ndago na kwekwe.
-
Usianzishe
kitalu kwenye sehemu yenye wadudu au magonjwa ama wanyama waharibifu
kama vile panya, nyani, tumbili n.k.
-
Eneo
la kitalu liwe na udongo wenye rutuba, unaohifadhi maji lakini usio
tuwamisha maji na udongo usiwe na chumvi chumvi
-
Eneo
la kitalu linatakiwa liwe tambarare, kama ni eneo la milimani, basi
ni muhimu kutengeneza matuta ya kitalu kwa kufuata matuta ya
mkingamo.
-
Kitalu
kinatakiwa kisiwe mbali sana na bustani halisi ya mboga ili
kurahisisha ubebaji na shughuli za kupandikiza miche.
-
Hakikisha
kitalu kipo karibu na njia ili kurahisisha kuleta mbolea, samadi au
mboji na pembejeo zingine.
-
Eneo
la kitalu liwe na urahisi wa kupata maji ya kutosha kwa ajili
umwagiliaji wa miche. Pawe na kisima au bwawa kwa ajili ya kuhifadhi
maji.
-
Eneo
liwe na miti kando kando ya kukinga upepo ili kuzuia upepo mkali
Kwenye kitalu.
-
Eneo
la kitalu liwe na mwanga wa jua wa kutosha.
Eneo
la kitalu lisiwe na magugu sugu kama vile ndago na kwekwe.
Usianzishe
kitalu kwenye sehemu yenye wadudu au magonjwa ama wanyama waharibifu
kama vile panya, nyani, tumbili n.k.
Eneo
la kitalu liwe na udongo wenye rutuba, unaohifadhi maji lakini usio
tuwamisha maji na udongo usiwe na chumvi chumvi
Eneo
la kitalu linatakiwa liwe tambarare, kama ni eneo la milimani, basi
ni muhimu kutengeneza matuta ya kitalu kwa kufuata matuta ya
mkingamo.
Kitalu
kinatakiwa kisiwe mbali sana na bustani halisi ya mboga ili
kurahisisha ubebaji na shughuli za kupandikiza miche.
Hakikisha
kitalu kipo karibu na njia ili kurahisisha kuleta mbolea, samadi au
mboji na pembejeo zingine.
Eneo
la kitalu liwe na urahisi wa kupata maji ya kutosha kwa ajili
umwagiliaji wa miche. Pawe na kisima au bwawa kwa ajili ya kuhifadhi
maji.
Eneo
liwe na miti kando kando ya kukinga upepo ili kuzuia upepo mkali
Kwenye kitalu.
Eneo
la kitalu liwe na mwanga wa jua wa kutosha.
Utayarishaji wa kitalu cha mboga
Mambo
muhimu ya kuzingatia
-
Fanya
usafi wa kina kwenye eneo ulilolichagua kwa kuondoa vichaka na
magugu yote.
-
Hakikisha
upatikanaji wa maji kwa kuweka mifereji au njia za kuleta maji au
kuhifadhi maji kwa kutengeneza kisima au mifereji.
-
Ni
vizuri kutenga eneo maalumu kwa ajili ya kuhifadhi na kuchanganya
mbolea.
-
Hakikisha
umelima na kutifua kwa jembe eneo lililotengwa kuoteshea miche.
-
Usisahau
Kuangamiza wadudu na magonjwa yatokanayo na udongo kabla ya
kutayarisha matuta ya kitalu kwa kutumia madawa ya kunyunyiza katika
udongo, kuchoma udongo au kufunika eneo la tuta la kitalu kwa
kutumia plastiki inayopitisha mwanga kwa wiki mbili hadi nne ili
kuua wadudu na minyoo udongoni.
Fanya
usafi wa kina kwenye eneo ulilolichagua kwa kuondoa vichaka na
magugu yote.
Hakikisha
upatikanaji wa maji kwa kuweka mifereji au njia za kuleta maji au
kuhifadhi maji kwa kutengeneza kisima au mifereji.
Ni
vizuri kutenga eneo maalumu kwa ajili ya kuhifadhi na kuchanganya
mbolea.
Hakikisha
umelima na kutifua kwa jembe eneo lililotengwa kuoteshea miche.
Usisahau
Kuangamiza wadudu na magonjwa yatokanayo na udongo kabla ya
kutayarisha matuta ya kitalu kwa kutumia madawa ya kunyunyiza katika
udongo, kuchoma udongo au kufunika eneo la tuta la kitalu kwa
kutumia plastiki inayopitisha mwanga kwa wiki mbili hadi nne ili
kuua wadudu na minyoo udongoni.
Aina za matuta ya kitalu
Kuna
aina tatu za matuta ya kitalu unayoweza kutengeneza kulingana na
msimu na aina ya udongo wa mahali ulipo, tuta la kitalu lililo inuka
(tuta n° 1) au tuta la kitalu lililo didimia au jaluba ( tuta n° 2)
ama tuta lililo inuka lakini lililobonyea kidogo katikati (tuta n°
3).
1.
Tuta lililoinuka na kubonyea katikati
Hili
hutumika wakati wa kiangazi sehemu zenye udongo mzito aina ya
mfinyanzi unaotuamisha maji ili husaidia kuhifadhi maji.
2.
Tuta lililoinuka
Hili
hutumika sehemu zenye unyevu na mvua nyingi au sehemu zenye udongo
mzito aina ya mfinyanzi unaotuamisha maji ili kuruhusu maji
kutawanyika na kwenda chini ya aridhi.
3.
Jaruba
Jaruba
hutumika sehemu kame au wakati wa kiangazi ili kuhifadhi unyevu wa
kutosha katika udongo kwa ajili ya miche.
Upandaji mbegu
2. Tuta lililoinuka
3. Jaruba
Upandaji mbegu
Kuna namna mbili za kupanda mbegu kwenye kitalu kama ifuatavyo.
1.
Kupanda kwa kutawanya katika tuta.
Kupanda
mbegu kwa kutawanya, hufanyika kwa mbegu ndogo ndogo sana kama za
mchicha. Ambapo kwa kawaida inashauriwa kuchanganya mbegu hizi na
mchanga (katika uwiano wa 1:4) kabla ya kupanda ili kusaidia kuwa na
mtawanyiko mzuri wa mbegu katika tuta zima. Baada ya kupanda pitisha
reki kuzifukia au mwaga mchanga kiasi juu ya tuta ili kuzifunika.
2.
Kupanda kwa mstari
Upandaji
wa mbegu kwa mstari unatakiwa kutengeneza mifereji inayo katisha
upana wa tuta kwa kutumia kijiti. Mfereji huu uwe na kina kisichozidi
sm 2 hadi sm 3. Kupanda mbegu ndogo ndogo kama vile vitunguu, nyanya
na kabichi tumia mifereji yenye kina cha sm 2 ili huepusha kuoza kwa
mbegu kama zikipandwa chini sana. Weka umbali wa sm 15 hadi 20 kati
ya mstari na mstari. Baada ya kupanda mbegu katika mstari rudishia
udongo na baadaye shindilia udongo ili uweze kushikana na mbegu
vizuri.
Mbegu zikishafunikwa kwa udongo, tandaza nyasi juu ya tuta
la kitalu ili kuzuia maji kupotea hewani na kukauka kwa tuta na mbegu
kabla na baada ya kuota. Kisha mwagilia maji kiasi na baada ya hapo
tuta limwagiliwe maji asubuhi na jioni kulingana na hali ya hewa na
aina ya udongo. Unaweza kumwagilia maji hadi mara tatu kwa siku kwa
sehemu zilizo na jua kali au udongo wa kichanga.
Kupanda mbegu kwa kutawanya, hufanyika kwa mbegu ndogo ndogo sana kama za mchicha. Ambapo kwa kawaida inashauriwa kuchanganya mbegu hizi na mchanga (katika uwiano wa 1:4) kabla ya kupanda ili kusaidia kuwa na mtawanyiko mzuri wa mbegu katika tuta zima. Baada ya kupanda pitisha reki kuzifukia au mwaga mchanga kiasi juu ya tuta ili kuzifunika.
2. Kupanda kwa mstari
Upandaji wa mbegu kwa mstari unatakiwa kutengeneza mifereji inayo katisha upana wa tuta kwa kutumia kijiti. Mfereji huu uwe na kina kisichozidi sm 2 hadi sm 3. Kupanda mbegu ndogo ndogo kama vile vitunguu, nyanya na kabichi tumia mifereji yenye kina cha sm 2 ili huepusha kuoza kwa mbegu kama zikipandwa chini sana. Weka umbali wa sm 15 hadi 20 kati ya mstari na mstari. Baada ya kupanda mbegu katika mstari rudishia udongo na baadaye shindilia udongo ili uweze kushikana na mbegu vizuri.
Mbegu zikishafunikwa kwa udongo, tandaza nyasi juu ya tuta la kitalu ili kuzuia maji kupotea hewani na kukauka kwa tuta na mbegu kabla na baada ya kuota. Kisha mwagilia maji kiasi na baada ya hapo tuta limwagiliwe maji asubuhi na jioni kulingana na hali ya hewa na aina ya udongo. Unaweza kumwagilia maji hadi mara tatu kwa siku kwa sehemu zilizo na jua kali au udongo wa kichanga.
Matunzo ya kitalu
Ondoa
nyasi juu ya kitalu mbegu zikishaota. Jengea kichanja kilichotandazwa
nyasi au makuti ama kitu chochote ili punguza kupenya kwa mionzi ya
jua kwa sababu miche hii bado ni michanga sana hivyo huathirika kwa
jua kali ambalo linaweza kuiunguza au kuifanya isikue vizuri.
Kichanja kiki kiwe na urefu wa mita moja ili kuwezesha ung’oaji wa
magugu na kupunguzia miche bila tatizo lolote. Kichanja hupunguza
kasi ya matone ya mvua kubwa ambayo inaweza kujeruhi miche michanga.
Kichanja cha kitalu kinaweza kukaa kwa muda wa wiki mbili. Punguza
kiasi cha kivuli cha matandazo ya nyasi pole pole na unaweza kutoa
kabisa baada ya wiki mbili au tatu.
Miche yenye majani mapana kama
vile, kabichi na nyanya, inahitaji kupunguziwa ili kutoa nafasi ya
kukua vizuri. Miche ihamishwe mapema maana kuhamisha miche mikubwa ni
vigumu zaidi kwa sababu mizizi yake ni mirefu na inaweza kukatika
kirahisi.
Utayarishaji
wa miche ya kupanda shambani
Ondoa
kivuli baada ya wiki mbili au tatu tangu kuota kwa miche ili husaidia
miche ianze kuzoea hali halisi ya bustanini hasa jua na upepo mkali.
Wiki moja kabla ya kupeleka miche bustanini yaani baada ya wiki
nne
kwa mazao mengi ya mboga (kasoro kitunguu wiki 5) punguza kiwango cha
maji ya kumwagilia ili miche izoee hali ngumu ya ukame baada ya
kupandikizwa bustanini. Miche ipandikizwe ikiwa na udongo kidogo
kuzunnguka mizizi yake ili iweze kushika vizuri mara baada ya
kupandikizwa shambani.
Miche yenye majani mapana kama vile, kabichi na nyanya, inahitaji kupunguziwa ili kutoa nafasi ya kukua vizuri. Miche ihamishwe mapema maana kuhamisha miche mikubwa ni vigumu zaidi kwa sababu mizizi yake ni mirefu na inaweza kukatika kirahisi.
Ondoa kivuli baada ya wiki mbili au tatu tangu kuota kwa miche ili husaidia miche ianze kuzoea hali halisi ya bustanini hasa jua na upepo mkali. Wiki moja kabla ya kupeleka miche bustanini yaani baada ya wiki
nne kwa mazao mengi ya mboga (kasoro kitunguu wiki 5) punguza kiwango cha maji ya kumwagilia ili miche izoee hali ngumu ya ukame baada ya kupandikizwa bustanini. Miche ipandikizwe ikiwa na udongo kidogo kuzunnguka mizizi yake ili iweze kushika vizuri mara baada ya kupandikizwa shambani.
UTHIBITI WA MAGONJWA NA WADUDU KATIKA MBOGA
Wadudu
na magonjwa hupunguza kiasi cha mavuno na hata kuua mimea kabisa,
Hupunguza ubora wa mboga, Huongeza gharama za uzalishaji, hasa madawa
ya viwandani yanapotumiwa na Huongeza uharibifu wa mboga baada ya
kuvuna.
Ni lazima utambue aina ya ugonjwa au mdudu ili utumie
kinga Ianayostahili kukabili. Ili kufanikisha lengo hili unaweza
kutumia uzoefu wako, hasa baada ya kuwa na wataalam wa wadudu na
magonjwa ya mimiea kwa muda mrefu, Kutumia mabwana shamba, Kutumia
wataalam wa magonjwa na wadudu wa mboga au kuchunguza sehemu ya mmea
uliyougua kwenye maabara.
Ni lazima utambue aina ya ugonjwa au mdudu ili utumie kinga Ianayostahili kukabili. Ili kufanikisha lengo hili unaweza kutumia uzoefu wako, hasa baada ya kuwa na wataalam wa wadudu na magonjwa ya mimiea kwa muda mrefu, Kutumia mabwana shamba, Kutumia wataalam wa magonjwa na wadudu wa mboga au kuchunguza sehemu ya mmea uliyougua kwenye maabara.
Kanuni za kukinga mboga dhidi ya magonjwa na wadudu
-
Panda
mazao muda unaotakiwa hii itakuwezesha kukwepa baadhi ya magonjwa ya
msimu.
-
Usipande
mboga ya jamii moja katika eneo moja kwa misimu mingi mfululizo.
Changanya mazao au mimea ambayo inafukuza magonjwa na wadudu kama
vile mimea inukayo
-
Chagua
udongo usiokuwa na magonjwa ya mboga unayotaka kuzalisha.
-
Tumia
mbegu bora, kwani baadhi ya magonjwa hutokana na mbegu.
-
Hakiksha
kuwa vitalu, bustani na sehemu ya kuhifadhi mboga ni safi kwani
uchafu na magugu huvutia magonjwa na wadudu waharibifu.
-
Hakikisha
unatoa majani au mimea iliyokwisha ugua, na ichome moto au ifukie..
-
Usichanganye
mboga na baadhi ya mazao yanayovutia magonjwa au wadudu katika
bustani yako. Mfano mazao kama mipapai na bamia huvutia nzi wadogo
weupe wanaoeneza ugonjwa wa "ukoma wa nyanya".
-
Tumia
madawa ya asili na viwandani ili kupunguza kuenea kwa magonjwa na
wadudu. Unalazimika kukinga mboga dhidi ya magonjwa na wadudu kwa
kutumia madawa ya asili na viwandani pale mbinu nyingine
zinaposhindwa kuleta mafanikio.
Panda
mazao muda unaotakiwa hii itakuwezesha kukwepa baadhi ya magonjwa ya
msimu.
Usipande
mboga ya jamii moja katika eneo moja kwa misimu mingi mfululizo.
Changanya mazao au mimea ambayo inafukuza magonjwa na wadudu kama
vile mimea inukayo
Chagua
udongo usiokuwa na magonjwa ya mboga unayotaka kuzalisha.
Tumia
mbegu bora, kwani baadhi ya magonjwa hutokana na mbegu.
Hakiksha
kuwa vitalu, bustani na sehemu ya kuhifadhi mboga ni safi kwani
uchafu na magugu huvutia magonjwa na wadudu waharibifu.
Hakikisha
unatoa majani au mimea iliyokwisha ugua, na ichome moto au ifukie..
Usichanganye
mboga na baadhi ya mazao yanayovutia magonjwa au wadudu katika
bustani yako. Mfano mazao kama mipapai na bamia huvutia nzi wadogo
weupe wanaoeneza ugonjwa wa "ukoma wa nyanya".
Tumia
madawa ya asili na viwandani ili kupunguza kuenea kwa magonjwa na
wadudu. Unalazimika kukinga mboga dhidi ya magonjwa na wadudu kwa
kutumia madawa ya asili na viwandani pale mbinu nyingine
zinaposhindwa kuleta mafanikio.
Kanuni za kukinga magonjwa na wadudu kwa kutumia madawa
Yafuatayonni
mambo ya kuzingatia wakati wa kutumia madawa ya asili na viwandani:
-
Usipige
dawa wakati wa upepo mkali au jua kali sana kwani kiasi kikubwa cha
dawa kinaweza kupotea hewani.
-
Usipige
dawa wakati wa mvua (mara tu kabla ya mvua) kwani maji ya mvua
yataosha na kupunguza nguvu ya dawa.
-
Unashauriwa
kupiga dawa wakati wa asubuhi hasa kukinga magonjwa ya ukungu
yapendayo unyevunyevu. Kwa kuzuia wadudu, ni vizuri kupiga dawa
wakati wa jioni. Wakati wa jioni dawa huua wadudu zaidi kwani hukaa
muda mrefu juu ya majani kabla ya nguvu yake kuharibiwa na jua.
-
Weka
kiwango cha dawa kama ilivyo elekezwa na watengenezaji au watalaam.
Kiasi kidogo cha dawa katika maji hufanya viini vya magonjwa na
wadudu kuwa sugu.
-
Kumbuka
kuwa kiasi cha sumu ndani ya kasha au kopo la dawa hutofautiana kati
ya kampuni na kampuni iliyotengeneza.
-
Ikiwezekana
tafuta ushauri kwa muuza madawa au wataalam waliokaribu nawe.
-
Hakikisha
unapiga dawa ya kutosha sehemu zote za mmea kwani baadhi ya wadudu
au magonjwa hukaa na kushambulia sehemu ya chini ya majani.
-
Andaa
vizuri bomba la kupigia dawa kabla ya kuchanaganya dawa na maji ili
dawa iweze kutoka vizuri.
-
Madawa
hutofautiana sana nguvu za kuua wadudu, hivyo changua madawa
yanayofaa kufuatana na ugonjwa na wadudu.
-
Unashauriwa
kupiga madawa hasa ya viwandani siku 14 kabla ya kuvuna mboga Pamoja
na kuepuka kupiga madawa mara kwa mara kwa usalama wa mlaji.
-
Epuka
Kupiga dawa ya aina moja mara kwa mara dhidi ya ugonjwa au mdudu wa
aina moja kwa sababu hii kufanya hivyo huwafanya wadudu kujenga sugu
dhidi ya dawa hiyo.
Usipige
dawa wakati wa upepo mkali au jua kali sana kwani kiasi kikubwa cha
dawa kinaweza kupotea hewani.
Usipige
dawa wakati wa mvua (mara tu kabla ya mvua) kwani maji ya mvua
yataosha na kupunguza nguvu ya dawa.
Unashauriwa
kupiga dawa wakati wa asubuhi hasa kukinga magonjwa ya ukungu
yapendayo unyevunyevu. Kwa kuzuia wadudu, ni vizuri kupiga dawa
wakati wa jioni. Wakati wa jioni dawa huua wadudu zaidi kwani hukaa
muda mrefu juu ya majani kabla ya nguvu yake kuharibiwa na jua.
Weka
kiwango cha dawa kama ilivyo elekezwa na watengenezaji au watalaam.
Kiasi kidogo cha dawa katika maji hufanya viini vya magonjwa na
wadudu kuwa sugu.
Kumbuka
kuwa kiasi cha sumu ndani ya kasha au kopo la dawa hutofautiana kati
ya kampuni na kampuni iliyotengeneza.
Ikiwezekana
tafuta ushauri kwa muuza madawa au wataalam waliokaribu nawe.
Hakikisha
unapiga dawa ya kutosha sehemu zote za mmea kwani baadhi ya wadudu
au magonjwa hukaa na kushambulia sehemu ya chini ya majani.
Andaa
vizuri bomba la kupigia dawa kabla ya kuchanaganya dawa na maji ili
dawa iweze kutoka vizuri.
Madawa
hutofautiana sana nguvu za kuua wadudu, hivyo changua madawa
yanayofaa kufuatana na ugonjwa na wadudu.
Unashauriwa
kupiga madawa hasa ya viwandani siku 14 kabla ya kuvuna mboga Pamoja
na kuepuka kupiga madawa mara kwa mara kwa usalama wa mlaji.
Epuka
Kupiga dawa ya aina moja mara kwa mara dhidi ya ugonjwa au mdudu wa
aina moja kwa sababu hii kufanya hivyo huwafanya wadudu kujenga sugu
dhidi ya dawa hiyo.
Madawa ya asili
Madawa
ya asili ni mengi ila bado hajafanyiwa utafiti wa kutosha kuhusu aina
ya wadudu na magonjwa ninayotibu, jinsi ya kutumia na kiasi cha
kutumia. Baadhi ya mimiea inayotoa madawa ya asili ni mbegu na majani
ya muarobaini, tumbaku, pilipili kali, pareto, kitunguu swaumu,
manung'anung'a, n.k. Muarobaini ni miongoni mwa mimea michahce ambayo
mpaka sasa imefanyiwa utafiti wa kiina. Mfano, kuchanganya nusu kilo
ya mbegu za muarobaini zilizotwangwa katika lita ishirini za maji
husaidia kuua wadudu mbalimbali wakiwemo funza wanaotoboa matunda ya
nyanya.
Madawa
ya asili ni bora zaidi kuliko madawa ya viwandani kwani sumu yake ni
kidogo na hupungua haraka baada ya kupiga dawa. Hivyo ni salama zaidi
kwa mpigaji dawa na mlaji mboga. Hivyo kupendekezwa katika kilimo hai
na hifadhi ya mazingira.
Kasoro
kubwa katika kutumia madawa ya asili ni kwamba hayajafanyiwa utafiti
wa kutosha ukilinganisha na yale ya viwandani. Mfano, nitumie dawa
ipi inayofaa kwa mdudu yupi?. Nguvu yake ni kidogo, hayatafaa kuzuia
mashambulizi makubwa ya magonjwa au wadudu vilevile yanakinga zaidi
mboga dhidi ya wadudu waharibifu kuliko magonjwa.Pia uwiano wa
kuchanganya dawa na maji bado haujulikani vizuri. Mfano, niweke kiasi
gani cha dawa katika kiasi gani cha maji ?..
Madawa ya viwandani
Madawa
ya viwandani yana sumu nyingi zaidi na hivyo huzuia haraka zaidi
mashambulio ya magonjwa na wadudu. Hivyo, hutumika sana katika kilimo
cha mboga na mazao mbali mbali kuliko madawa ya kienyeji. Changamoto
la haya madawa ni kwamba ni hatari kwa mkulima, mlaji wa mboga,
mazingira na pia gharama zake ni kubwa.
KUVUNA NA KUHIFADHI MBOGA
Uvunaji wa mboga
Uvunaji
wa mazao ya mboga ni hatua ya mwisho na muhimu sana katika
uzalishaji. Kabla ya kuchukua uamuzi wa kuvuna mboga ni muhimu
kufanya utafiti wa soko la mavuno hayo, kutafakari na kuchagua aina
au njia ya kuvuna na kusafirisha mazao hadi kwenye soko. Ni muhimu
kupanga mipango hii mapema ili pindi zao linapokomaa uvunaji ufanyike
na hivyo kuepuka zao kubakia bustanini kwa muda mrefu ambao
utasababisha kuharibika.
Unapaswa
kuwa makini sana katika mipangilio ya shughuli zake ili kujipatia
mavuno mengi na bora na baadaye kuweza kuyauza kwa bei nzuri.
Jinsi
ya kutambua ukomavu unaofaa kwa kuvuna mboga za aina mbali
mbali.
Dalili au kipindi cha ukomavu unaofaa kwa kuvuna mboga
maranyingi hutokana na uzoefu wa mkulima mwenyewe pamoja na mahitaji
ya soko, umbali wa kusafirisha mboga na aina ya usafiri utakao tumika
kusafirisha mboga. Kumbuka kuwa mboga ni mazao yasiyoweza kuhifadhika
kwa muda mrefu na yanahitaji kutumiwa haraka mara tu baada ya
kuvunwa.
Dalili au kipindi cha ukomavu unaofaa kwa kuvuna mboga maranyingi hutokana na uzoefu wa mkulima mwenyewe pamoja na mahitaji ya soko, umbali wa kusafirisha mboga na aina ya usafiri utakao tumika kusafirisha mboga. Kumbuka kuwa mboga ni mazao yasiyoweza kuhifadhika kwa muda mrefu na yanahitaji kutumiwa haraka mara tu baada ya kuvunwa.
Uvunaji wa mboga mboga
Dalili
za mboga iliyo tayari kuvunwa inategemea aina ya zao lenyewe. Kwa
mfano mboga za majani kama vile mchicha, chainizi kabichi, inatakiwa
iwe na majani teke yasiyo komaa sana. Mchicha usiwe umeanza kutoa
hata lile ua la kwanza. Chainizi ivunwe kabla ya majani yake kuwa na
miiba/manyoya na pia majani hayatakiwi kutoa nyuzi yanapochunwa.
Uvunaji
wa kabichi
Kabichi
inafaa ivunwe wakati ikiwa imefunga vizuri na kuwa ngumu inapo
kubonyezwa kwa kidole gumba. Pia iwapo utaipiga kwa mkono inatoa mlio
wa ngoma. Kabla ya kuonyesha dalili hizi basi kabichi itakuwa bado
haijakomaa. Na madhara yake ni kunyauka mapema baada ya kuvunwa.
Uvunaji
wa mboga za matunda
Uvunaji
wa Mboga za matunda kama vile ngogwe, biringanya na bamia zivunwe
wakati ngozi yake ikiwa ni ng'aavu na laini. Hapo mbegu zilizomo
ndani bado hazijakomaa na hivyo ni laini kwa kula. Baadaa ya hapo
hugeuka rangi na kuwa njano (mfano ngogwe na biriganya) au kupoteza
ung'aavu wake. Hapo mbegu huwa zimekomaa na hazifai tena kwa soko.
Wakati mwingine uvunaji wa biringanya au ngogwe unaweza kufanyika
zingali changa, hii yaweza kufanyika kama kuna mahitaji maalum ya
mteja wa mboga ya aina hii. Hapo unaweza kumvunia mteja kwa
makubaliano.
Uvunaji
wa nyanya uko katika aina mbili:
(1)
Unaweza kuvuna nyanya mbichi kidogo kwa ajili ya mahitaji maalum ya
mteja au kama unasafirisha mbali na hivyo ziweze kufika zikiwa na
hali nzuri na kuiva taratibu safarini pasipo kuharibika.
(2) Unaweza
kuvuna nyanya zilizo iva kabisa, hizi zivunwe kama soko ni la karibu
au kwa mauzo ya hapo hapo ili kuepuka uharibifu safarini na mara
zikiwa sokoni.
Mazao
ya mbogamboga za mizizi
Mazao
ya mboga za mizizi kama vile karoti yavunwe yakiwa teke lakini
yamekomaa, kabla ya kuwa na nyuzi nyuzi au kamba kamba. Karoti iwe
imefikia ukubwa unao takiwa na kabla haija jaza maji na kupoteza
utamu au sukari. Sehemu ya katikati ya karoti isiwe kubwa na isiwe
imejaa maji.
Mboga
zinazovunwa zinatakiwa ziwekwe mahali penye kivuli cha kutosha na
unyevu pasipo na jua kali ili zisinyauke. Inapendekezwa, mboga
zivunwe kipindi cha asubuhi na siyo wakati wa jua kali. Isipokua
mboga jamii ya vitunguu ambavyo huhitaji kukaushwa ili kuhifadhika
vizuri.
(1) Unaweza kuvuna nyanya mbichi kidogo kwa ajili ya mahitaji maalum ya mteja au kama unasafirisha mbali na hivyo ziweze kufika zikiwa na hali nzuri na kuiva taratibu safarini pasipo kuharibika.
(2) Unaweza kuvuna nyanya zilizo iva kabisa, hizi zivunwe kama soko ni la karibu au kwa mauzo ya hapo hapo ili kuepuka uharibifu safarini na mara zikiwa sokoni.
Uhifadhi wa mboga
Jinsi
ya kuhifadbi mboga baada ya kuvuna
Unaweza kupunguza kuharibika
kwa mazao ya mboga kwa njia zifuatazo
-
Unatakiwa
kuvuna mboga mbichi asubuhi na mapema kabla jua halijawa kali ili
kupunguza uharibifu utokanao na joto kali linalo sababishwa na jua.
-
Hakikisha
unaosha mboga zako mara baada ya kuvuna ili kupunguza joto la jua,
hasa endapo umevuna wakati wa jua kali.
-
Hakikisha
unahifadhi mboga mahali pasafi ili kuepuka maambukizo ya magonjwa ya
kuozesha mboga.
-
Hifadhi
mboga zilizovunwa katika sehemu ya baridi au kivuli na yenye unyevu
wa kutosha. Hata hivyo vitunguu huhitaji kuhifadhiwa sehemu kavu ili
visiote.
-
Wakati
wa kusafirisha, panga mboga katika vyombo imara vyenye ujazo mdogo
mfano wa makasha, badala ya kushindilia katika matenga, magunia,
viroba au kumwaga katika gari/lori.
-
Epuka
kupakia mboga kupita kiasi katika matenga au magari ya kusafirishia
ili hupunguza mgongano au mbanano wa mboga ambao unaweza kusababisha
vidonda na kuoza kwa mboga haraka.
-
Nyunyizia
maji kwenye mboga hasa mboga za majani ili zisinyauke na kuharibika
haraka.
Unaweza kupunguza kuharibika kwa mazao ya mboga kwa njia zifuatazo
Unatakiwa
kuvuna mboga mbichi asubuhi na mapema kabla jua halijawa kali ili
kupunguza uharibifu utokanao na joto kali linalo sababishwa na jua.
Hakikisha
unaosha mboga zako mara baada ya kuvuna ili kupunguza joto la jua,
hasa endapo umevuna wakati wa jua kali.
Hakikisha
unahifadhi mboga mahali pasafi ili kuepuka maambukizo ya magonjwa ya
kuozesha mboga.
Hifadhi
mboga zilizovunwa katika sehemu ya baridi au kivuli na yenye unyevu
wa kutosha. Hata hivyo vitunguu huhitaji kuhifadhiwa sehemu kavu ili
visiote.
Wakati
wa kusafirisha, panga mboga katika vyombo imara vyenye ujazo mdogo
mfano wa makasha, badala ya kushindilia katika matenga, magunia,
viroba au kumwaga katika gari/lori.
Epuka
kupakia mboga kupita kiasi katika matenga au magari ya kusafirishia
ili hupunguza mgongano au mbanano wa mboga ambao unaweza kusababisha
vidonda na kuoza kwa mboga haraka.
Nyunyizia
maji kwenye mboga hasa mboga za majani ili zisinyauke na kuharibika
haraka.
Sababu za mboga kuharibika
-
Umbali
kati ya masoko na sehemu ya uzalishaji.
-
Ubovu
wa miundombinu ya usafirishaji kama barabara na upungufu wa vyombo
vya usafiri.
-
Msuguano
au mbanano ambao husababisha mikwaruzo na vidonda kwenye mboga. Hii
husababishwa na kupakia mboga kupita kiasi na bila mpangilio katika
matenga au magunia.
-
Joto
kali na hewa kavu ya kuhifadhi husababisha mboga mbichi kupoteza
maji mengi sana na hata kunyauka kabla ya kuuzwa.
-
Mashambulizi
ya magonjwa na wadudu mbalimbali baada ya kuvuna husababisha mboga
kuharibika au kuoza.
-
Namna
mbaya ya Upangaji na upakiaji wa mboga katika vyombo vya
kusafirishia.
Umbali
kati ya masoko na sehemu ya uzalishaji.
Ubovu
wa miundombinu ya usafirishaji kama barabara na upungufu wa vyombo
vya usafiri.
Msuguano
au mbanano ambao husababisha mikwaruzo na vidonda kwenye mboga. Hii
husababishwa na kupakia mboga kupita kiasi na bila mpangilio katika
matenga au magunia.
Joto
kali na hewa kavu ya kuhifadhi husababisha mboga mbichi kupoteza
maji mengi sana na hata kunyauka kabla ya kuuzwa.
Mashambulizi
ya magonjwa na wadudu mbalimbali baada ya kuvuna husababisha mboga
kuharibika au kuoza.
Namna
mbaya ya Upangaji na upakiaji wa mboga katika vyombo vya
kusafirishia.
Upangaji wa mboga katika vyombo vya kusafirishia
Unashauriwa
kupanga mboga vizuri katika vyombo vya kusafirishia ili kupunguza
uharibifu wa mboga kwa njia ya mgandamizo na msuguano na kuruhusu
mzunguko mzuri wa hewa na hivyo kupunguza uwezekano wa kuoza kwa
mboga. Vile vile kupanga vizuri mboga hufanya bidhaa kuvutia zaidi
wateja.
Aina za vyombo/vifaa vya kusafirishia mboga
Unashauriwa
kuchagua vifaa vya kuhifadhia mboga kufuatana na upatikanaji na
gharama za vyombo hivyo, aina ya mboga na usafiri.
1. Makasha
ya mbao au plastiki huweza
pia kutumika badala ya matenga kuhifadhia mboga zinazoharibika haraka
zaidi kama vile nyanya, pilipili hoho, n.k. Makasha ni mazuri kwani
hupunguza uharibifu wa mboga unaotokana na mbanano kati ya kasha na
kasha. Pia kwa kuwa makasha yanamatundu, husaidia kupunguza joto kali
ndani ya kasha na mboga.
2. Magunia, viroba
na mapakacha hufaa zaidi kwa mboga zote ambazo haziharibiki haraka
kama vile vitunguu, vitunguu swaumu, kabichi, ngogwe, karoti, viazi
vitamu na mviringo, n.k.
3. Matenga hufaa
kutumika kusafirishia mboga ambazo huharibika haraka kama vile
nyanya, bilinganya, ngogwe, chainizi, swisichardi, pilipili hoho,
n.k. Licha ya kuwa na matundu ya hewa (kupunguza joto), hata hivyo
matenga siyo mazuri kusafirishia mboga laini kwani husababisha
uharibifu mkubwa wa mboga kutokana na mgandamizo kati ya tabaka na
tabaka na pia kati ya tenga na tenga.
1. Makasha ya mbao au plastiki huweza pia kutumika badala ya matenga kuhifadhia mboga zinazoharibika haraka zaidi kama vile nyanya, pilipili hoho, n.k. Makasha ni mazuri kwani hupunguza uharibifu wa mboga unaotokana na mbanano kati ya kasha na kasha. Pia kwa kuwa makasha yanamatundu, husaidia kupunguza joto kali ndani ya kasha na mboga.
2. Magunia, viroba na mapakacha hufaa zaidi kwa mboga zote ambazo haziharibiki haraka kama vile vitunguu, vitunguu swaumu, kabichi, ngogwe, karoti, viazi vitamu na mviringo, n.k.
3. Matenga hufaa kutumika kusafirishia mboga ambazo huharibika haraka kama vile nyanya, bilinganya, ngogwe, chainizi, swisichardi, pilipili hoho, n.k. Licha ya kuwa na matundu ya hewa (kupunguza joto), hata hivyo matenga siyo mazuri kusafirishia mboga laini kwani husababisha uharibifu mkubwa wa mboga kutokana na mgandamizo kati ya tabaka na tabaka na pia kati ya tenga na tenga.
Madaraja ya ubora wa mboga
Haya
huitwa pia 'gredi'. Kupanga mboga katika gredi ni muhimu sana hasa
katika masoko ya ushindani. Husaidia kufanya bidhaa ivutie zaidi
wateja na hivyo basi kuuzika kirahisi.
Vigezo
vya kutumia wakati wa kugredi mboga
Vigezo
hivi viko vingi na vinategemea hali ya soko la mboga. Vigezo vikuu ni
kama ifuatavyo.
-
Ukubwa
wa matunda, majani, viazi, vitunguu au karoti.
-
Rangi
ya matunda na majani.
-
Usafi
wa mboga. Mboga zilizooshwa huvutia zaidi wateja.
-
Maumbile
ya matunda au tunguu.
-
Kiwango
cha ukomavu wa matunda.
Vigezo hivi viko vingi na vinategemea hali ya soko la mboga. Vigezo vikuu ni kama ifuatavyo.
Ukubwa
wa matunda, majani, viazi, vitunguu au karoti.
Rangi
ya matunda na majani.
Usafi
wa mboga. Mboga zilizooshwa huvutia zaidi wateja.
Maumbile
ya matunda au tunguu.
Kiwango
cha ukomavu wa matunda.
KILIMO CHA MATONE (DRIP IRRIGATION)
Hii
ni njia ya kumwagilia mmea kwa kutumia tone(matone) la maji kwa muda
husika, ambapo bomba dogo huundwa kwa kuwekewa matundu madogo madogo
kwa kuzin¬gatia mmea ulipo kwaajili ya kuupa maji mmea muda wote,
Umwagiliaji huu unaweza kuendeshwa kwa mashine au kwa mkono.
Umwagiliaji huu pia unaweza fanyika kwa mazao yaliyo mengi ikiwemo ya
mboga mboga, matunda na hata nafaka. Katika maeneo yaliyo mengi
umwagiliaji huu wakulima hupendelea kuufanya kwa mazao ya matunda na
mboga mboga.
Faida za umwagiliaji wa matone
-
Mgawanyo
wa maji katika mimea ni sawa.
-
Mmonyoko
wa udongo ni mdogo sana.
-
Hupunguza
gharama za wasaidizi shambani.
-
Huokoa
muda.
-
Matumizi
ya maji ni yenye mafanikio.
-
Mavuno
ni ya uhakika
Mgawanyo
wa maji katika mimea ni sawa.
Mmonyoko
wa udongo ni mdogo sana.
Hupunguza
gharama za wasaidizi shambani.
Huokoa
muda.
Matumizi
ya maji ni yenye mafanikio.
Mavuno
ni ya uhakika
Mambo ya kuzingatia kabla ya kuanza umwagiliaji wa matone
Aina
ya udongo.
Aina
ya udongo ni muhimu sana kujua aina kama ni tifutifu, kichanga au
mfinyanzi,hii itakusaidia mkulima kujua uwezo wa aina husika ya
udongo wa kuhifadhi maji ardhini.
Nafasi
katika upandaji.
Kila
zao lina nafasi zake katika upandaji hivyo unavyoweka mfumo wa
umwagiliaji hakikisha nafasi unazo weka ziendane na nafasi ya zao
husika.
Topografia
Huu
ni umwagiliaji wenye mafanikio hakikikisha eneo lako lipo tambarare,
hata kama mteremko utawepo uwe mteremko wa wastani, kufanya mgawanyo
wa maji kuwa sawa. Pia zingatia sehemu ya kuweka chanzo cha maji
inaweza kuwa ni pipa liliweke¬wa miundo mbinu mizuri miundombinu
hiyo kama bomba zilizo sanifiwa vyema kufikia kwenye mmea, pipa au
chanzo chochote cha maji hicho kiwekwe sehemu iliyo inuka ili kufanya
maji yateremke vizuri kwenye bomba mpaka kwenye mmea.
Mgawanyo
wa maji.
Maji
ni lazima yawe yenye ubora na maji yawe ya uhakika, kwa kuzingatia
hilo pia topografia ya eneo husika ni iwe tambarare au mteremko kiasi
Kuruhusu maji ku gawanyika vyema kwenye mmea kwa kiwango kile kile na
spidi ile ile kwa kila mmea.
Aina ya udongo ni muhimu sana kujua aina kama ni tifutifu, kichanga au mfinyanzi,hii itakusaidia mkulima kujua uwezo wa aina husika ya udongo wa kuhifadhi maji ardhini.
Nafasi katika upandaji.
Kila zao lina nafasi zake katika upandaji hivyo unavyoweka mfumo wa umwagiliaji hakikisha nafasi unazo weka ziendane na nafasi ya zao husika.
Huu ni umwagiliaji wenye mafanikio hakikikisha eneo lako lipo tambarare, hata kama mteremko utawepo uwe mteremko wa wastani, kufanya mgawanyo wa maji kuwa sawa. Pia zingatia sehemu ya kuweka chanzo cha maji inaweza kuwa ni pipa liliweke¬wa miundo mbinu mizuri miundombinu hiyo kama bomba zilizo sanifiwa vyema kufikia kwenye mmea, pipa au chanzo chochote cha maji hicho kiwekwe sehemu iliyo inuka ili kufanya maji yateremke vizuri kwenye bomba mpaka kwenye mmea.
Mgawanyo wa maji.
Maji ni lazima yawe yenye ubora na maji yawe ya uhakika, kwa kuzingatia hilo pia topografia ya eneo husika ni iwe tambarare au mteremko kiasi Kuruhusu maji ku gawanyika vyema kwenye mmea kwa kiwango kile kile na spidi ile ile kwa kila mmea.
Changamoto za umwagiliaji wa matone
Kama
maji yatakayo tumika katika umwagiliaji yakiwa na chumvi husababisha
udongo kuwa na chumvi. Kama miundombinu haitawekwa sawa upotevu wa
maji utakuwa mkubwa.
Jinsi ya kuweka mfumo wa umwagiliaji shambani
Vitu
vifuatavyo viwepo; vifaa, chanzo cha maji,ukubwa wa shamba. Katika
umwagiliaji huu vifaa vinavyoweza tumika ikiwemo,
i.Chanzo
cha maji
kinaweza
kuwa pipa, hakikisha pipa hili limetobolewa na kupitisha maji mpaka
kwenye bomba ambazo zitakuwa zimewekwa moja kwa moja kwenye mmea.
ii.Bomba
Hizi
ziwe zimetobolewa kulingana na nafasi kutoka mmea hadi mmea, na
zimewekwa kulingana na mstari kama mistari ipo kumi na bomba ziwe
kumi. Sehemu za mfumo huu wa umwagiliaji
ii.Vali(valvu)
Kazi
ya hichi chombo ni kuruhusu maji yatoke au yasitoke, ni sawa sawa na
koki kama wengine wanavyoita.
iii.Kichujio
Ni
muhimu sana kwani itasaidia kuchuja maji kuzuia uchafu kama mchanga,
nyasi ambazo huenda zikasabibisha matundu yakutolea maji kuziba, hizi
chujio ziwek¬we kabla ya kufungwa bomba za kupeleka maji kwenye
mmea.
iv.Emmita:
Haya
ndio matundu ambayo yanapeleka maji kwenye mmea, kwa kawaida hutoa
maji kwa muda wa saa moja kwa maji lita 4 kwa gallon moja la maji.
i.Chanzo cha maji
kinaweza kuwa pipa, hakikisha pipa hili limetobolewa na kupitisha maji mpaka kwenye bomba ambazo zitakuwa zimewekwa moja kwa moja kwenye mmea.
ii.Bomba
Hizi ziwe zimetobolewa kulingana na nafasi kutoka mmea hadi mmea, na zimewekwa kulingana na mstari kama mistari ipo kumi na bomba ziwe kumi. Sehemu za mfumo huu wa umwagiliaji
ii.Vali(valvu)
Kazi ya hichi chombo ni kuruhusu maji yatoke au yasitoke, ni sawa sawa na koki kama wengine wanavyoita.
iii.Kichujio
Ni muhimu sana kwani itasaidia kuchuja maji kuzuia uchafu kama mchanga, nyasi ambazo huenda zikasabibisha matundu yakutolea maji kuziba, hizi chujio ziwek¬we kabla ya kufungwa bomba za kupeleka maji kwenye mmea.
iv.Emmita:
Haya ndio matundu ambayo yanapeleka maji kwenye mmea, kwa kawaida hutoa maji kwa muda wa saa moja kwa maji lita 4 kwa gallon moja la maji.