FAHAMU KUHUSU KILIMO HAI CHA MPUNGA

Share:


Chagua aina ambazo zinafaa kutumika katika mazingira husika. Mpunga hujipevusha wenyewe. Hii inaruhusu kuchagua mbegu kutoka shambani kwako mwenyewe.
 Tenga kilo 30 hadi 40 za mbegu kwa ajili ya kupanda hekta 1

Kabla ya mbegu kuchipua
Anza kutayarisha mbegu kabla ya mvua kuanza. Mbegu zinazotoka kuhifadhiwa miezi 3 au zaidi zinahitaji kwanza kupashwa joto kwenye jua kwa masaa 3.

Ruhusu mbegu zipoe kabla ya kuziloweka kwa siku 1. Baada ya hapo Ondoa mbegu zinazoelea. Jaza mbegu nusu kiroba kwa ajili ya kuvundika kwa masaa 36. Kagua mbegu mara kwa mara ili joto lisipande sana.

NAMNA YA KULIMA NA KUWEKA MBOLEA
- Tengeneza matuta kupunguza upotevu wa udongo.
- Epuka usumbuaji wa ardhi usio wa lazima.
- Boresha rutuba na hifadhi ya udongo kwa kilimo mseto kwa kutumia mazao yatakayokuwa mbolea za kijani.
- Zuia upungufu wa virutubisho kwa kuongeza mbolea za kilimo hai na fospheti ya mawe
-Zuia ushindani wa magugu na mbegu zake kuongezeka kwa kufanya palizi ya mara kwa mara kwa muda sahihi.

KUVUNA
Vuna pale tu mpunga utakapokuwa umekomaa.
Kupanda aina mchanganyiko kunaweza kusababisha shamba moja likawa na viwango tofauti vya kukomaa vya kukomaa.
Tandaza nafaka zisilundikane wakati wa kukausha kuzuia kuvu.
Tumia mashine sahihi za kukoboa ili kuhakikisha asilimia kubwa ya punje za mchele zinatoka nzima.
Mchele unatakiwa usiwe na makapi, mbegu za magugu na mawe ili kupata bei nzuri.