Choroko
ni zao la chakula na biashara lenye kiasi kikubwa cha protini na
madini ya phosphorus na calicium. Zao hili likilimwa vizuri hutoa
mavuno kati ya Kg 400 hadi 900 kwa ekari moja.
UDONGO
NA HALI YA HEWA IFAAYO
Choroko
hustawi katika udongo wa aina tofauti usiotuamisha maji. Hulimwa
kutoka mita 0 hadi 1500 kutoka usawa na bahari japokuwa kuna mbegu
nyingine zinaweza kukubali zaidi ya ukanda huu. Hili ni zao
linalostahimili ukame.
AINA
ZA CHOROKO
Kuna
aina kuu mbili za choroko ambazo pia zimegawanyika katika makundi
mawili,choroko nyeusi na choroko za kijani.
1.
CHOROKO ZINAZOTAMBAA-hizi ni choroko ambazo zinarefuka sana na
hutambaa sehemu mbalimbali.
2.
CHOROKO ZINAZOSIMAA-Hizi ni choroko ambazo zinakuwa kwa kusima
kwenda juu.Hizi huchukua muda mfupi kukomaa wastani wa siku 60-70.
KIPINDI
KIZURI CHA UPANDAJI WA CHOROKO
Choroko
hazihitaji maji mengi hivyo ni budi zipandwe mwishoni mwa msimu wa
mvua,Pia zinaweza kupandwa katika shamba lililolimwa mpunga.
NAFASI
ZA UPANDAJI WA CHOROKO NA KIASI CHA MBEGU
Choroko
huitaji mbegu kiasi cha kilogram 8 hadi kumi kwa ekari moja.
Panda
choroko zako kwa nafasi ya sentimeta 30 mastari na mstari na
sentimeta 10 shina hadi shina (30 x10 )sentimeta au (40 x 8
)sentimeta.
SAMADI
NA MBOLEA ZA VIWANDANI
Kama
shmba lako halina rutuba ya kutosha unaweza kuongeza samadi kiasi cha
tani tano kwa ekari na pia unaweza kupanda kwa kutumia mbolea ya NPK
kg 50 kwa ekari.weka mbolea zote kabla ya kupanda.
UMWAGILIAJI
Kama
umepanda kipindi cha ukame sana au unalima kilimo cha umwagiliaji
basi mwagilia shamba lako upate unyevu wa kuotesha mbegu, kisha baada
ya mbegu kuota kaa siku 6 hadi 10 na umawgilie tena. Mara tatu za
kumwagilia zinatosha kwa choroko.
PALIZI
Palilia
shamba lako mapema kuzuia magugu.Palizi moja inaweza kutosha.
MAGONJWA
YA CHOROKO
1.
Yellow mosaic virus ( Ugonjwa wa manjano)
Dalili:
mmea unakuwa wa njano na madoa ya njano katika majani.
Kinga
na tiba-Panda mbegu zinazostahimili magonjwa.
2.
Powdery Mildew (Ukungu)
Dalili-Majani
yanakuwa na vidoti vya njano ambavyo vinabadilika kuwa vya kahawia au
kijivu haraka na ambapo kunakuwa na unga unga katika majani.
Kinga
na tiba-Panda mbegu zinazostahimili ukungu,Pulizia dawa za ukungu
(Fungicide).
anza
kupuliza wiki tatu baada ya mimea kuota na kuendelea kulingana na
hali halisi.
3.
LEAF SPOT (Vidoti katika majani)
Dalili-majani
yanakuwa na vidoti vya mviringo na visivyo na umbo maalum ambapo
katikati yanakuwa na rangi rangi ya kijivu na weupe na mistari
ya rangi ya wekundu-kahawia au nyeusi-kahawia.ugonjwa huu husababisha
hasara hadi ya asilimia 58 ya mapato.
Kinga
na Tiba-Panda mbegu inayostahimili ugonjwa huu,Choma mabaki ya mimea
hii na ile ya jamii moja baada ya kuvuna.Pulizia dawa za ukungu
(Fungicide) Katika nafasi ya wiki mbili mbili kama eneo hilom
linashambuliwa mara kwa mara na ukungu.
WADUDU.
Kuna
wadudu mbalimbali wanaoshambulia choroko kama vile aphidi,funza wa
vitumba,nzi wa maharage.Wazui wadudu hawa kwa kupuliza dawa za wadudu
mara tu baada ya mimea kuota,dawa kama karate,twigathoate,dimethote
na nyinginezo zinaweza kutumika.
UVUNAJI
Mara
tuu choroko zinapofikia asilimia 85 ya ukaukaji zinabidi zivunwe
ukichelewa zitapukutikia shambani.