FAHAMU KUHUSU KILIMO HAI CHA KOROSHO

Share:

koroshoo ni zao ambalo chimbuko lake ni Portuguese na baadae karne ya 16 ndipo lilipo fika africa katika nchi ya msumbiji na baadae likafika nchini Kenya na Tanzania.
Tanzania korosho hulimwa na kustawi vizuri katika mikoa ya kusini Mtwara, lindi, na maeneo kama Mafia, bagamoyo na Rufiji.
Kiwango cha mvua
korosho ustawi vizuri kwenye maeneo yenye mvua 840mm - 1250 mm wastani wa mvua kwa mwaka,napia hukua vizuri kwenye maeneo 0- 500 m kutoka usawa wa bahari.
udongo ufaao
korosho ukua vizuri kwenye maeneo yenye PH 5.6 udongo wa kichanga (sandy) na pia udongo mfinyazi kichanga.
Maandalizi ya shamba
shamba la korosho linatakiwa kusafishwa, kusawazishwa nakutifuliwa vizuri kwaajili ya kupanda korosho. ashimo utakayo chimba unaweza kuweka mbolea ya ngombe ukachanganya na udongo mapema ili kuongeza rutuba.
Upandaji
baada ya kununua mbegu unachukua maji na chumvi 100g ya chumvi unaweka katika maji kiasi cha lita 5 unakoroga vizuri na unachukua mbegu zako unaweka kwenye maji hayo zile zitakazo zama ndio mbegu zenye uwezekano mkubwa wa kiota, baada ya hapo unazianika vizuri hili ziweze kukauka.
Aina za upandaji wa korosho
njia ya kitaru
hii ni njia ni nzuri kwa sababu unakua huru kuchagua mche ambao umestawi na ulio na muonnekano mzuri , unatakiwa kuamishia miche shambani ikiwa na umri wa wiki 6 na zingatia kuchagua mche wenye afya Na baadae unatakiwa kupunguza majani urefu wa sm60- 90 kutoka kwenye ardhi na pia ondoa majani yote ambayo yanaonekana kuadhiliwa na magonjwa au wadudu na yale yalio kauka.
MAGONJWA NA WADUDU
MAGONJWA
- Anthracnose
- powdery mildew

WADUDU
coconut bug
trips aphids
Cashew stem girdler
heliotropes bug
cashew weevil
meal bug
namna ya kuzuia wadudu na magonjwa
Palilia mapema
Weka shamba katika hali ya usafi
Tumia mbinu ya kuchanganya mazao kwa korosho unaweza kuchanya pamba au maharage hiyo inasaidia kukimbiza wadudu wengine ambao wanakua hawapatani na mazao hayo
Uvunaji
Korosho ufikia hatua ya kuzaa matunda pale inapo kua na umri wa miaka 2 1/2 hadi miaka mitatu
Pia matunda ukomaa pale inapo kua na miaka 9 hadi 10
Uwezekano wa mkoroso kuishi ni miaka 30 hadi 40
matumizi ya korosho
chakula 
hutumika kutengeneza rangi
Hutumika kama zao la biashara
miti yake hutumkia kama kuni
kutengeneza dawa