FAIDA YA TUNDA LA APPLE KWA AFYA YA BINAFSI

Share:

Tunda hili lina faida kubwa katika mwili wa mwanaadamu. Na faida za tunda la apple ni kama zifuatazo.

Maumivu ya kichwa
Tunda hili lina faida katika maumivu ya kichwa. Apple lilowiva unatakiwa ulimenye maganda yake, halafu ule kwa kutia chumvi kidogo kila siku asubuhi kabla ya kula kitu chochote, na uendelee kufanya hivi kwa muda wa wiki mbili.

Anaemia
Tunda la apple lina madini ya iron, arsenic na phosphorus, kwa mtu mwenywe ugonjwa huu inafaa kutengeneza juice ya apple . Inashauriwa kunywa glass mojaya juisi ya apple kabla kula chakula (nusu saa kabla) na pia kabla ya kwenda kulala usiku.

High Blood Pressure
Apple linasaidia katika kuongeza kutoa (secreation) mkojo ambapo husaidia kurudisha blood pressure katika hali ya kawaida, pia inasaidia kupungua kwa sodium chloride katika figo.

Dysentery
 Kwa watoto wanaosumbuliwa na maradhia ya ghlabu , inashauriwa kumpa kila wakati kipande cha apple kwani huzuia hali ya ugonjwa huo.

Meno
kila baada chakula kula apple moja, maana tunda hili husaidia sana kuyasafisha na kuyaepusha meno na vijidudu na kuoza.

Matatizo ya tumbo
 Kuna matatizo tofauti ya tumbo, kwahivo tunda hili limekusanya matatizo yote ya tumbo na kuondoa matatizo hayo. Changanya apple, asali kidogo na ufura kidogo na kula kabla chakula hiki husaidia kuondoa matatizo ya tumbo kama vile usagaji mdogo wa chakula na mengine.

Kuharisha na kutapika
 Mwenye kutokezewa na ugonjwa huu ni vizuri sana kutumia tunda hili na Kila siku ale mawili pia kama yatapikwa au kuchomwa ni mazuri zaidi kwani hulainisha cellulose.