KILIMO HAI CHA MCHICHA

Share:


Mchicha ni mboga za majani ambazo zina katika miili yetu.
Hali ya hewa na udongo
Mchicha unahitaji maji ya kutosha wakati wa kupanda hadi kuvuna. mchicha huhitaji udongo wenye rutuba ya kutosha na wenye kuhifadhi maji.
Utayarishaji wa shamba.
Tengeneza shamba la mchicha kwa kutifua ardhi na kulainisha udongo wenye kina cha sentimeta thelathini. Weka mbolea ya samadi debe moja katika kila mita moja ya mraba. Panda mchicha katika matuta yenye upana wa 90cm-100cm.

Aina ya mbegu
- Amaranthus hypochondriacus ni mchicha wenye majani ya kijani na mbegu zake ni njano.
- Amaranthus hybridus huu ni mchicha wenye majani mekundu na mbegu zake ni nyeusi.
- Amaranthus dubius ni mchicha wa kienyeji na Aspinosus ni mchicha wenye miba mingi.
- Amarantus africana ni mchicha wenye majani ya kijani na mbegu zake ni ni nyeusi.
Upandaji
- Mchicha upandwe katika tuta kwa mistari yenye nafasi ya sentimita thelathini.
    - Funika mbegu kwa kutumia udongo uliolaini na tandaza nyasi kavu baada ya kupanda ili kutunza unyevunyevu.
    - Pandikiza mchicha kwa nafasi ya sentimeta kumi na tano kwa ishirini.
    - Mwagilia maji ya kutosha.
    Mbolea
Tumia mbolea ya samadi iliyolowekwa kwenye maji kwa muda wa masaa ishirini na nne kumwagilia mchicha wako ili kupata mavuno mengi zaidi. Tumia kiasi cha debe moja kwa kila mita moja ya mraba.
wadudu waaribifu
wadudu aina ya mafuta au kitaalamu zaidi huitwa spinach aphids ambao hufyonza utomvu wa mchicha na kusababisha majani kujikunja , mchicha kusinyaa na kunyauka.
Pia mdudu aina kitambazi hula majani ndani kwa ndani
Namna ya kudhibiti wadudu
mwagilia mchicha wako kutumia chombo kinachotoa maji mithili ya mvua kitaalamu kinaitwa "watering can" ili kuwadondosha wadudu aina ya spinach aphids katika mchicha.
Kwa mdudu aina kitambazi tumia mwarobani kunyunyuzia majani ili kuwaua wadudu hao waharibifu.
Mavuno
Mchicha huwa tayari kuvunwa baada ya majuma 3 hadi 6 tangu kupandwa au kupandikizwa.
Kiasi cha mavuno
Kila mita moja ya mraba huzalisha kiasi cha 4kg hadi 5kg za mchicha. Hii inamaanisha kuwa utapata kiasi cha tani 20 hadi 40 kwa hekta moja ya mchicha.
NAMNA YA KUHIFADHI MCHICHA
Vuna mchicha wako kisha usafishe vizuri

    - Funga katika mafungu.
    - Chemsha maji mpaka yachemke.
    - Tumbukiza mafungu ya mchicha katika maji yanayochemka kwa muda wa dakika 1 hadi 2.
    - Kausha vizuri chini ya kivuli na utunze mchicha wako katika sehemu isiyo na unyevunyevu.