Faida ya kula la parachichi

Share:

Parachichi ni aina ya kipekee ya tunda. Tafiti mbalimbali zilizofanyika zimebaini kuwa tunda la parachichi limesheheni manufaa makubwa katika afya ya mwanadamu.

 Faida ya kula tunda la parachichi ni kama zifuatazo
Hulinda afya ya moyo
Madini ya potasiamu yanayopatikana kwenye tunda la parachichi kwa zaidi ya asilimia 14 ni muhimu sana katika utendaji kazi wa misuli ya moyo. 
Huzuia saratani
Tafiti zilizofanyika zimebainisha kuwa kula matunda ya parachichi kunasaidia kupunguza kasi ya ukuaji wa seli za saratani ya tezi dume. 
Lehemu mbaya hupunguzwa
Utafiti unaonyesha kuwa watu wanaokula parachichi kiwango chao cha lehemu mwilini ni tofauti na wale wasiokula kabisa.Wingi wa mafuta ya lehemu inaweza kuleta matatizo ya moyo.
Virutubisho mbalimbali
Parachichi ni tunda la pekee ambalo limebeba virutubisho mbalimbali ambavyo ni muhimu kwa ajili ya miili yetu. Baadhi ya virutubisho vinavyopatikana kwenye parachichi ni:
  • Asidi ya Folate: asilimia 20
  • Kalori 240 (184 inatokana na mafuta)
  • Vitamini K: asilimia 26
  • Vitamini E: asilimia 10
  • Miligramu 11 za sodiamu
  • Vitamini C: asilimia 17
  • Gramu 13 za wanga
  • Vitamini B5: asilimia 14
  • Gramu 10 za nyuzinyuzi za lishe
  • Gramu 1 tu ya sukari
  • Potasiamu asilimia 14
  • Vitamini B6: asilimia 13

Huzuia uvimbe
Waatalamu wamebainisha Asidi ya Oleic inayopatikana kwenye parachichi, husaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia uvimbe mwilini.

Huimarisha mifupa
Tunda la parachichi lina nafasi kubwa katika kuimarisha mifupa kutokana lina vitamini K pamoja na madini ya kopa na folate ambavyo ni muhimu kwa ajili ya mifupa.

Afya ya Ubongo
Kama unahitaji afya ya ubongo wako katika hali nzuri, inashauriwa kutumiwa matunda ya parachichi kwasababu madini ya kopa yanayopatikana kwenye parachichi yana nafasi kubwa sana katika kufanya ubongo ufanye kazi vyema. 

Ongezeko la nguvu ya mwili
Mwili wa binadamu hutegemea sana wanga, protini na mafuta ili kupata nguvu. Pia ukila tunda la parachichi itawezesha kuongeza nguvu katika mwili wako. 

Uboreshwaji wa mmeng'enyo wa chakula
Vyakula vyenye nyuzinyuzi ni muhimu sana kwa ajili ya kuufanya mmeng’enyo wa chakula uende vizuri. Parachichi ni tunda lenye nyuzinyuzi kwa karibu asilimia 13 ambazo ni sawa na kiwango cha asilimia 54 unachotakiwa kula. Je bado huoni umuhimu wa tunda hili? Anza kula ili uboreshe mmeng’enyo wako wa chakula sasa.
Ni nzuri kwa wajawazito
Kuwepo kwa kiasi kikubwa cha folate, potasiamu, Vitamini C na B6 ambazo ni muhimu kwa ajili ya afya na ukuaji wa mtoto; kunalifanya tunda la parachichi kuwa na umuhimu mkubwa kwa wajawazito.
Hivyo inashauriwa wanawake wajawazito wazingatie ulaji wa matunda hasa tunda la parachichi.