KILIMO CHA CHAI

Share:
UTANGULIZI
Chai inasemekana ilianza kulimwa China na kusambaa japan, indonesia, india,malawi,uganda,
 sri lanka na kenya na Tanzania

Tanzania chai inalimwa sana sana bukoba, iringa, kilimanjaro, mbeya na njombe. Inasemekana Tanzania ni nchi ya nne kwa uzalishaji wa chai Africa baada ya kenya, Malawi na Uganda, Inazalisha kama tani 32000 kwa mwaka.

AINA YA CHAI
kuna aina mbili za chai
ASSAM TEA hii aina ya chai hulimwa maeneo ya baridi pia nimikubwa na ukilinganisha na china tea
CHINA TEA aina hii ya chai ina urefu wa mita 6 na pia inakua polepole, ni mifupi na ina majani ya kijani iliyo koza

MAZINGIRA
- Chai hustawi katika maeneo yenye mvua kiasi 1500-2500mm lakini inaweza kukua pia katika maeneo ambapo hakuna mvua kubwa ya 1200 mm

JOTO
kilimo bora cha chai kinafaa kwenye maeneo ya joto la18 – 20°C 

MVUA  
. Kiasi cha mvua kinachohitajika 1500 - 1750mm ndani ya mwaka
 . Mvua ndefu husababisha mmonyoko wa udongo

UDONGO
. Chai inakuwa kwenye udongo wenye asili ya Volcano 

. Udongo unatakiwa uwe na urefu kwenda chini (1.8 - 2.0m), unyevu wa kutosha 

. Udongo uwe na rutuba na pia chai ilimwe kwenye udongo wa acid (optimum PH-value 4.0 -6.0) Chagua kitalu kizuli, eneo la kitalu liwe limewekwa vizuri kwa ajili ya kupinguza kasi ya upepo pia liwe eneo ambalo jua linafika ili kuwezesha mimea inayo kua kupata mwanga wa jua. 
Udongo wa kitalu
- Udongo wa juu unatakiwa kua na PH 5.5 na udongo wa chini PH5 na pia udongo unatakiwa na rutuba ya kutosha

KUANDAA SHAMBA
Ardhi ambayo haijawai kulimwa ndio inayo faa zaidi eneo ambalo limeshalimwa linatakiwa kusafishwa kwa kuondoa visiki ili kuzuia magonjwa ya mizizi.
• magugu yote yanatakiwa kuondolea  na mashimo ya kupandia hua yanatakiwa kua na upana was m 30 na urefu was m 45.
Nafasi ya kupanda ni 1.5m mmea kwa mmea  na 0.75m kati ya msitari kwa mstari au 1.2m mmea kwa mmea au o.9m mstari kwa mstari  ambayo hukitumia nafasi hiyo utapata  mimea 8000- 9000 /ha

BAADA YA KUPANDA
 • chai mda mwingine hupandwa kwenye kitalu
KUWEKEA NYASI. •kuwekea nyasi husaidia katika kutunza unyevu na kuzuia mmomonyoko na kuzuia magugu kuota kwa kasi. Hakikisha nyasi unazoweka hazigusi mche .unaweza kuweka nyasi kwa kuzungushia mche.

MBOLEA
Mbolea ya viwanda ndio inafanya vizuri kwenye zao la chai zaidi ya mbolea za asili, na kiasi cha kuweka mbolea  nikama ifuatavyo.
Nitrogeni • Nitrogen nimbolea ambayo ni muhimu sana kwenye zao la chai. Katika mwaka wa  kwanzana wapili  weka ½  na rudia ¾ ya kiasi kinacho itajika. Na unatakiwa kuweka mbolea yenye nitrogen kuanzia mda wa miezi mitatu. Unaweza kutumia NPK. 
Mbolea ya kukuzia  usitumie CAN kwa sababu Ca inazuia mmea kuchukua K yaani Potassium.

KUZUIA MAGUGU
Mmea mdogo- katika mimea midogo hua hua viua gugu hutimka zaidi unaweza kutumia viua gugu kama hii uhua magugu mengi ya muda mrefu na aina mazara katika udongo
viua  gugu hivyo sio kwamba huua magugu kwa asilimia 100 il unaweza kutumia mfano kupruni  kumbuka kuondoa magugu yote kabla ya kupanda. 
Katika mimea mikubwa • magugu huzuiwa na kuweka kivuli pamoja na kuweka nyasi(mulching) lakini pia viua gugu vinaweza kutumika pia.

UMWAGILIZIAJI
Kumwagiliza wakati wa kiangazi au ukame n I muhimu sana

KULINGANISHA MIMEA NA KUPLUNI 
Hii ni muhimu sana kwa sababu inawezesha mmea kua na shape zuli pamoja na urefu unao staili.

WADUDU
Wadudu wanao hathiri sana chai ni kama ifuatavyo
 (i)Helopeltis bugs (Helopeltis schoutedeni)  
 (ii) Black Citrus Aphid (Toxoptera aurantii)
.  Termites
African field cricket
Scales Tea borer
Unaweza kuzuia kibaologia kwa kutumia wadudu wa   African weaver ants  au kwa kutumia mti wa neem  au kwa kutumia viua dudu.

MAGONJWA
(i) Armilaria root Rot (Armillariella mellea) 
 Back Root Rot (Rosellinia arcuata)
Brach and colour Canker, brown and grey blight
grey blight brown blight
Brach and colour Canker
Unaweza kuzuia wadudu kwa kutumia viua dudu.

KUVUNA
Chai huvunwa kwa kukwanyua , kuvunwa hua unavuna skwa enterval ya siku 10  au siku 6 hadi 14 inategemea na hali ya hewa. Mda wa kuvunwa kuanzia mda wa kupanda inategemea na njia ulio tumia kupanda yaani unavuna baada ya miaka 2 kama ulitumia njia ya kukata na miaka 4 kama ulitumia mbegu.

Kwa mwaka unaweza kuvuna 1000 -1300 kg/ha  kwa  chai ambayo  imesindikwa  na mara 5 yake ya majani ya kijani  chini ya usimamizi mzuri, na ukiwa na mtu mwenye uzofu wa kuvuna anaweza kuvuna 30 kg kwa siku.