FAHAMU KWA UNDANI KUHUSU KILIMO CHA ZABIBU

Share:
HISTORIA YA KILIMO CHA ZABIBU
Kilimo cha Zabibu mkoani Dodoma kina historia ndefu, ambapo kwenye miaka ya 1950 na mwaka 1974 chini ya uzaidizi wa bihwana misheni, serikali ya Tanzania wakati huo ikishirikiana na serikali ya china ilianzisha kituo cha kilimo cha Bihawana Farmers Training Center (BFTC) kwa ajili ya kufundisha Wakulima juu ya kilimo cha Zabibu na mazao mengine.

Dodoma ndio mkoa pekee unaolima Zabibu kwa wingi nchini Tanzania na hata kwa afrika mashariki ndio mkoa wenye utajiri mkubwa wa zao hili.

Maeneo yanayolimwa Zabibu mkoani Dodoma
Hali ya hewa ya Dodoma inaruhusu zao hili kustawi katika maeneo mengi mkoani hapa,baadhi ya maeneo yanayolimwa Zabibu ni Mpunguzi, Mbabala, Hombolo, Chamwino, Bahi, Mvumi, Msalato, Gawaye .
Ramani ya mkoa wa Dodoma: uzalishaji mkubwa unafanywa katika wilaya ya Dodoma mjini, ikifuatiwa na chamwino na Bahi.

AINA YA ZABIBU
kuna aina tatu za Zabibu ambazo ni Zabibu za mvinyo,Zabibu za mezani na Zabibu za kukausha ambazo zote zinazalishwa Dodoma. Zabibu zinazozalishwa sana Dodoma ni za mvinyo zikifuatiwa na za mezani.

HALI YA HEWA
Kilimo cha zabibu kinahitaji mvua za wastani japokuwa dodoma inajulikana kwa ukame ila ardhi yake ina hifadhi maji kwa kipindi kirefu sana kwahiyo kwa mvua zinazonyesha kuanzia desemba mpaka machi zinatosha kwa kuhudumia mizabibu mpaka mwezi wa julai kulekea kipindi cha mavuno.

MAGONJWA YA MIZABIBU

Ugonjwa wa Ubwiri Poda (Powderymildew)
Ugonjwa huu huenea zaidi vipindi vya joto/ukame. Ugonjwa huu hushambulia zaidi mazao kama Zabibu, nyanya, hoho n.k. Majani huwa na madoadoa ya njano ambayo huambatana na poda nyeupe chini ya jani.

Ugonjwa wa Kinyaushi (Dampingoff)
Ugonjwa wa Kinyaushi husababishwa na vimelea vya ukungu jamii ya (Pythium, Rhizoctoniasolani, Phytophthoraspp na Sclerotium). Ukungu huu au vimelea vya ukungu wa aina hii huishi kwenye udongo.

Mimea inayoshambuliwa au kuhifadhi ugonjwa huu ni mingi mno na husababisha mnyauko wa miche ya mazao mengi shambani. Mmea uliopatwa na ugonjwa huu huwa mwembamba sanamithili ya waya hasa kwenye shina. Mara nyingine ugonjwa wa aina hii huozesha mche hata kabla ya mche kustawi vizuri

Ukungu wa kuchelewa(Lateblight)
Huu ni ugonjwa wa Zabibu pia ambao kama haukudhibitiwa husababisha madhara kiasi cha karibu asilimia 90-100 ya mavuno. Ugonjwa huu husababishwa na vimelea vya ukungu jamii ya Phytophthorainfestans ambayo hutokea zaidi vipindi vya baridi kali na mvua.

Jinsi ya kupambana na magonjwa ya fangasi:
- Hakikisha unatembelea shamba lako mara 3 hadi 4 kwa wiki, au ikiwezekana kila siku. Unatakiwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara, hakikisha unazunguka shambani, kagua mimea yako kwenye majani juu na chini pamoja na shina. Uchunguzi wa mara kwa mara utasaidia kujua kwa haraka dalili za ugonjwa kabla ya kuleta madhara.

- Hakikisha usafi wa shamba lako kuanzia wakati wa upandaji hadi baada ya kuvuna. Hakikisha palizi inafanyika kwa wakati, maana baadhi ya magugu hutumika kama mazalia ya vimelea vya fangasi, pia magugu shambani husababisha unyevunyevu ambao hustawisha fangasi. Na si hivyo tu magugu pia
huficha wadudu ambao ni waharibifu kwa mimea lakini pia wadudu hao hutumika kusambaza magonjwa hayo ya fangasi

- Piga dawa zisizo kuwa na kemikali kwa wakati hasa katika kipindi cha masika,na hakikisha unatumia dawa sahihi. Mbali na magonjwa hayo ya fangasi pia kuna magonjwa yanayosababishwa na wadudu, kama nzi,mbung’o,funza wa vitumba 

UVUNAJI WA ZABIBU
Mzabibu mpya unachukua miezi nane ndio huanza kuzaa na unakuwa hafifu, inapofikia miaka mitatu uzao wake huongezeka maradufu na vifaa vinavyohitajika kwa uvunaji ni mikasi,kisu,kreti/ndoo.

Muda wa mzuri wa kuvuna Zabibu ni asubuhi kwa kuwa muda huu jua linakua sio kali,hivyo itasaidia kupunguza matunda mengi kuanguka chini wakati wauvunaji,na pia mvunaji atakua akivuna kwa utaratibu bila kero yoyote ya jua.