Faida za Karanga Mbichi kwenye mwili wa mwanadamu
KINGA DHIDI YA KIHARUSI
Ugonjwa hatarishi wa kiharusi ambao unasumbua watu wengi nchini Tanzania unaweza kujingika nao kwa kula karanga mbichi
Utafiti umeonesha kuwa karanga ina kirutubisho aina ya Resveratrol ambacho hupatikana pia kwenye zabibu na mvinyo mwekundu (red wine). Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa maabara na
kuchapishwa kwenye jarida la Kilimo na Kemia ya Chakula (Journal of Agricultural Food Chemistry), umeonesha kuwa kirutubisho hicho huimarisha utembeaji wa damu kwenye mishipa inayokwenda kwenye ubongo kwa kiasi cha asilimia 30.
MAGONJWA YA MOYO
karanga ni chanzo kizuri cha mafuta mazuri aina ya
monounsaturated fats ambayo ni mazuri kwa afya ya moyo. Kwa mujibu wa utafiti, watu wanaokula karanga mara kwa mara hupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo (cardiovascular heart disease).
Aidha, katika taarifa iliyochapishwa kwenye jarida moja la Uingereza la Journal of Nutrition
ambako kuna matokeo ya taarifa nne za utafiti,imeonesha pia watu wanaotumia karanga mara kwa mara, angalau mara nne kwa wiki, hujipa kinga nyingine dhidi ya ugonjwa wa moyo (coronary heart disease) kwa zaidi ya asilimia 37.
KINGA DHIDI YA KANSA YA TUMBO .
Faida nyingine inayoweza kupatikana kwenye mwili kutokana na ulaji wa karanga, ni kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya tumbo.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, unaonesha kuwa virutubisho vya folic acid, phytosterols,
phytic acid (inositol hexaphosphate) na resveratrol vinavyopatikana kwenye karanga,
huweza kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya tumbo.
Utafiti huo umeonesha kuwa ulaji wa karanga, hata mara mbili tu kwa wiki, una uwezo
wa kupunguza uwezekano wa kupatwa na saratani ya tumbo kwa asilimia 58 kwa wanawake na asilimia 27 kwa wanaume!