Soya ni zao jamii ya mikunde ambayo ina baadhi ya sifa za mbegu zinazozalisha mafuta. Zao la soya lina protini nyingi yenye ubora wa hali ya juu kuliko iliyoko katika aina nyingine ya mazao ya mimea.
HALI YA HEWA NA UDONGO
Soya ni zao linalostahimili ukame na huweza kulimwa kwenye maeneo yenye mvua kidogo, kwenye mvua za wastani soya hufanya vizuri kwenye udongo wa tifutifu na kwenye udongo wa mfinyanzi.
Mvua
Soya huhitaji wastani wa mvua ya mililita 350 hadi 1,500 za mvua kwa mwaka na inayonyesha kwa mtawanyiko. Soya pia inafaa katika kilimo cha umwagiliaji kwani katika maeneo hayo kunakuwa na uhakika wa unyevu muda wote.
KUANDAA SHAMBA
Utayarishaji wa shamba la soya ni lazima uondoa magugu yote kwa kuwa soya haivumilii magugu hasa ikiwa katika hatua za mwanzo za ukuaji (seedling stage).
Shamba la soya linaweza kulimwa kwa sesa au matuta. Kilimo cha sesa chaweza kulimwa kwa kutumia jembe la mkono au la kukokotwa na wanyama kazi kama maksai na punda au kwa kutumia trekta. Kilimo cha matuta kuzuia mmomonyoko wa udongo na kupunguza kasi ya maji kinafaa na kinapendekezwa kwa maeneo yenye mwinuko.
NAMNA YA KUPANDA UPANDA
Maeneo yenye mvua nyingi Soya huanza kupandwa mwishoni mwa mwezi Novemba mpaka katikati ya mwezi Desemba na Maeneo yenye mvua kidogo alizeti hupandwa mwezi February hadi March.
Jambo la kuzingatia wakati wa kupanda ni kuhakikisha kuwa mbolea haigusani na mbegu kwa sababu mbolea itaunguza mbegu na hazitaota.
- Mkulima anashuriwa kupanda soya kwa nafasi zinazo pendekezwa na wataalamu. Nafasi hizo ni sentimeta 10 kwa sentimita 45 kwa soya fupi kama bossier na kwenye sehemu zenye rutuba hafifu.
- Sentimeta 10 kwa sentimita 60 kwa soya ndefu kama UyoleSoya1 na kwenye sehemu zenye rutuba nyingi.
- Panda mbegu moja kila shimo na zifukiwe kwa kina cha sentimeta mbili hadi sentimita 5 ili zisiharibiwe au kuliwa na wanyama kama panya.
Wataalamu wanashauri mkulima ahakikishe kuwa soya inapandwa kwenye udongo wenye unyevu wa kutosha; haitakiwi kabisa kupanda soya kwenye udongo mkavu au kuloweka soya kabla ya kupanda.
KIASI CHA MBEGU
Ni muhimu kuandaa mbegu bora na safi mapema kabla ya msimu wa mvua kuanza. Kwa wastani kilo 20 hadi 30 za mbegu za soya zinatosha kwa hekta moja kutegemeana na aina ya mbegu. Kwa kuwa aina nyingi za soya hazistawi kila mahali, ni muhimu kwa mkulima kuhakikisha kuwa anatumia mbegu inayofaa katika eneo analotaka kulima soya hususani mahitaji ya mvua
MBOLEA
soya pia huhitaji udongo wenye rutuba na usiotuamisha maji ili iweze kustawi. soya huhitaji wastani wa kilo 80 hadi 100 za mbolea aina ya DAP na TSP kwa hekta moja na kilo 60 hadi 80 kwa mbolea aina ya CAN kwa hekta moja (Heka 2 na Nusu).
NAMNA YA KUZUIA MAGUGU
mkulima anashauriwa kuwahi palizi katika kipindi cha wiki mbili baada ya soya kuota.
WADUDU,MAGONJWA NA VIUMBE WANAOSHAMBULIA SOYA
WADUDU WAHARIBIFU
wadudu watatokea mkulima anashauriwa kutumia dawa za wadudu kama Thiodan 35% EC na Sumithion 50% EC kwenye kipimo cha mililita 40 za dawa na lita 20 za maji au kipimo kinacho pendekezwa katika dawa husika. Upuliziaji wa dawa ufanywe kulingana na kiasi cha mashambulizi ya wadudu kwenye mazao.
MAGONJWA
Magonjwa ambayo hutokea kwenye zao la soya ni vimelea vya ukungu na bakteria. Magonjwa haya huenezwa kwa mbegu, masalia ya mimea shambani na wadudu mafuta.
Njia mojawapo ya kuzuia kuenea kwa magonjwa hayo katika zao la soya ni kupanda mbegu safi na zilizopendekezwa mahali husika. Aidha, panda kwa mzunguko (crop rotation) kwa kutumia mazao yasiyoshambuliwa na magonjwa ya soya kama alizeti na mahindi.
WANYAMA WAHARIBIFU
Soya hupendwa sana na panya wa shambani na ghalani. Wanyama wengine ni pamoja na sungura, Ngedere n.k.
Mkulima anashauriwa kutumia mbinu na njia mbalimbali zikiwemo za asili, kukabiliana na wanyama hao bila kuharibu mazingira.
UVUNAJI WA SOYA
DALILI ZA KUKOMAA
Dalili za soya kukomaa ni wakati majani yanapokuwa na rangi ya njano na huvunwa baada ya majani kuanza kupukutika.
NJIA ZA UVUNAJI
Baada ya soya kupukutisha majani shambani mkulima anatakiwa kung’oa soya kwa kutumia mikono au anaweza kuvuna kwa kutumia mashine maalumu za kuvunia.