ZIJUE MBINU NZURI ZA KILIMO BORA CHA CHOROKO

Share:

Choroko ni zao la chakula na biashara lenye kiasi kikubwa cha protini na madini ya phosphorus na calicium. Zao hili likilimwa vizuri hutoa mavuno kati Kg 400 hadi 900 kwa ekari 

AINA ZA CHOROKO
Tafiti zilizofanywa na wataalam wetu hapa Tanzania, zinaonyesha kuwa aina mbili za choroko ambazo ni IMARA na NURU  ndizo zenye kutoa mazao mengi zaidi.
Imara
Aina hii huchukua muda wa takribani siku 60-65 kukomaa na pia inao uwezo wa kuzaa kiasi cha tani 1.5-1.8 katika shamba la hekta moja (sawa na magunia 6-7 kwa ekari). Mbegu za Imara ni nene kuliko zile za Nuru. 
Nuru
Aina hii hukomaa ndani ya siku 55-60 huku ikiwa na uwezo wa kutoa kiasi cha tani 1.5-1.8 kwa hekta moja (magunia 6-7 kwa ekari). Rangi yake ni ya kijani na inang’ara. 
Udongo na Hali ya hewa 
Choroko hustawi katika udongo wa ianatofauti tofautiu usiotuamisha maji. Hulimwa kutoka mita 0 hadi 1500 kutoka usawa wa bahari japokuwa kuna mbegu nyingine zinaweza kukubali zaidi ya ukanda huu. Jili ni zao linalostahimili ukame
Muda wa kupanda
Kwa mujibu wa wataalamu wa kilimo wanashauri choroko zipandwe shambani miezi miwili kabla ya mvua kumaliziaka. Zinaweza kupandwa wakati wa vuli na masika pia.
Namna ya kupanda
Namna ya kupanda ni umbali wa sentimita 50 kutoka mstari hadi mstari na sentimita 10 kutoka shina hadi shina.
Palizi
 ili mimea ikuwe katika hali ya afya,hakikisha shamba lako linakuwa safi wakati wote ili kupata virutubisho vyote muhimu na pia kupunguza uwezekano wa kutokea kwa magonjwa au wadudu.
Uvunaji
 Zao la choroko lapaswa kuvunwa wakati limekauka vyema kabisa na iwe kabla ya vitumba havijaanza kupasuka kwa sababu ya jua huko shambani.