Faida za Kula Tunda la Embe

Share:
Embe ni tunda linalofahamika na kupendwa na watu wengi. Watu hula tunda hili moja kwa moja au kulitumia kutengeneza sharubati (juice).
faida za kula tunda la embe ni kama zifuatazo;
Madini ya potasiamu yanayopatikana kwenye embe huasidia dosari zinazosababishwa na madini ya sodiamu katika damu. Potasiuam hurekebisha nguvu ya msukumo wa damu (blood pressure) na kuufanya uwe wa kawaida.
Huboresha uwezo wa kumbukumbu
Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika jarida la Oxidative Medicine and Cellular Longevity, unaeleza kuwa embe lina vitamini B6 pamoja na asidi ya glutamine ambavyo vyote kwa pamoja huboresha afya ya ubongo.
Huboresha afya ya macho
Kula embe kutakunufaisha kwa kulinda macho yako dhidi ya kudhoofu kwa misuli ya macho. Embe ni chanzo kizuri cha vitamini A ambayo ni muhimu kwa ajili ya macho.
Huongeza asidic ya folic
Asidi ya folic inayopatikana kwenye embe katika mfumo wa vitamini B ni muhimu sana kwa afya ya mama mjamzito na mtoto. Inashauriwa na wataalamu wa afya kula tunda la embe hasa kwa wajawazito.
Hupunguza lehemu mwilini (cholesterol)
Kiwango cha mafuta ya lehemu kikizidi ni hatari kwa ajili ya afya ya moyo. Vitamini C pamoja na pectin inayopatikana kwenye embe huuwezesha mwili kujikinga na athari za lehemu.
Huboresha afya ya ngozi
Embe ni muhimu kwa ajli ya afya ya ngozi kwani lina beta-carotene ambayo mwili huibadili kuwa vitamini A na lina vitamini C kwa wingi ambazo zote kwa pamoja ni muhimu kwa ajili ya afya ya ngozi.
Husaidia kukabiri kisukari
Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa ulaji wa embe huweka kiwango cha mwili cha sukari na insulini katika hali nzuri.
Husaidia kukabili maradhi ya shambulio la moyo
Madini ya potasiamu yanayopatikana kwenye embe ni muhimu kwa ajili ya afya ya misuli ya moyo. Hivyo kunywa sharubati (juice) ya embe au kula matunda ya embe mara kwa mara kutakukinga na hatari ya maradhi ya shambulio la moyo.
Huboresha mmeng'enyo wa chakula
Embe lina enzyme ambazo husaidia katika uvunjwaji na uchakatwaji wa protini mwilini. Pia kama nilivyosema pale awali kuwa embe lina nyuzinyuzi ambazo ni muhimu katika kumeng’enya chakula.
Huboresha kinga ya mwili
Kinga mwili inahitaji vitamini A na C ili kujijenga na kujiimarisha. Hivyo ulaji wa matunda ya embe utakupatia vitamini hizi zinazopatikana kwenye matunda haya kwa wingi.