Faida ya maji ya dafu ni kama zifuatazo
(i) Maji ya madafu yana utajiri mkubwa sana wa vitamin mbalimbali, amino acids,vimengenyo, viondoa sumu pamoja na virutubisho mbalimbali.
(ii) Maji ya madafu yana imarisha mzunguko wa damu mwili
(iii) .Maji ya madafu yanasaidia kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili.
Yanazuia Upungufu wa Maji Mwilini.
(iv) Maji ya madafu yanasaidia kuzuia muonekano wa kizee (anti-aging ): Matumizi ya mara kwa mara ya maji ya madafu yatakufanya uonekane na kijana hata kama umri wako umeenda. Kuwa na uwezo wa kuzuia muonekano wa uzee ni miongoni mwa sababu zinazo yafanya maji ya madafu yawe maarufu sana miongoni mwa wasanii wanao igiza filamu katika huko Hollywood nchini Marekani.
(v) Maji ya madafu yana kiasi kidogo cha kalori.
(vi) Maji ya madafu yanasaidia kuimarisha mfumo wa usagaji chakula tumboni.
(vii) Maji ya madafu yanasaidia kukukinga dhidi ya magonjwa ya moyo pamoja na presha.
(viii) Yanaimarisha ubongo na misuli.