Dengu ni zao la chakula na biashara lenye kiasi kikubwa cha protini, vitamini A na B, Madini ya Potassium na chuma. Zao hili likilimwa vizuri linaweza kutoa mavuno ya kilogram 200 hadi 500 kwa ekari. Zao hili huchukua wastani wa siku135 kupandwa hadi kuvunwa.
Mambo ya kuzingatia
- Kuwa makini na hali ya hewa ya mwaka husika kwa kuangalia ukame katika mbuga utaaisha lini pia hali ya mvua ikoje kwa maana kuwa msimu wa kulima huwa mwezi wa tatu mwishoni kwenye maeneo ambayo mbuga huwahi kukauka mapema yaani muda huo ndiyo watu huanza kuandaa shamba kwa kulilima mara ya kwanza kama hatua ya kukiandaa shamba pia hatua hii hufanyika mwezi wa nne lakini iwe kwenye kumbukumbu sahihi kuwa dengu kwa hali ya uzuri kabisa hulimwa mwezi nne na mwanzoni kabisa mwa mwezi wa tano kabla mbegu hazichakauka .
- Uchaguzi wa Mbegu bora za dengu ni muhimu kuzifahamu na kuzitumia katika kilimo hiki Ziko mbegu ambazo hazihimili magonjwa lakini zipo zinazohimili magonjwa na zinakuwa na uzito hii husaidia katika swala la uuzaji kwa maana ya kuwa mara nyingi dengu kwa sasa huuzwa kwa kilo ili mkulima apate faida zaidi.
- Baada ya kulima mara ya kwanza unapaswa kulima mara ya pili na kupanda mbegu kwa kufata misitari au kufata vitalu au misingi imeadaliwa.
- Hakikisha dengu unapanda katika mbunga isiyo na maji yaliyotuama , unyevunyevu wa udogo wa shambani ndiyo hitaji muhimu la uoteshaji dengu hairuhusiwi kabisa kupanda dengu kwenye shamba lenye maji.
- Ardhi inayofaa kwenye kilimo cha dengu ni shamba lenye udongo mweusi ambao hutumika pia katika kilimo cha mpunga, mahidi, choroko na mengineyo .
- katika ulimaji wa dengu palizi haina ulazima mara nyingi dengu haina palizi kabisa ukizigatia hatua za mwanzo za uandaaji wa shamba
- Dengu hutumia miezi mitatu mpaka kuvuna hivyo inajulazimu kusubiri ikauke mpaka hali ujano itokee kwenye mmea, mavuno ya dengu mara zato hufanyika kwa kung’oa mmea wote na kukusanya sample dogodogo ili kumaliza mapema mavuno yake baada ya hatua hiyo unaleta mkokoteni shambani unajusanya kwa mkokoteni nakupeleka sehemu kavu iliyosafi kwa ajili ya kutoa maganda ya zao la dengu,hatua ya kutoa maganda ya dengu inaweza fanyika kwa kienyeji kwa kupiga na miti au ikatumika kwa kitaalamu kwa kupiga .
CHAGAMOTO KATIKA KILIMO CHA DENGU
- Wakati wa kupanda huwa kunachagamoto ya mvua ambazo hujitokeza na kuharibu zao la dengu kwa kisukuma tunaita SHIBOJA yaani mvua za kuozesha dengu chagamoto hiyo ikijitokeza subiri maji yakauke katia mbengu upya kama zao limeathiriwa kidogo kama limeathiriwa sana unarudia shamba lote.
- Chagamoto ya panya Panya hujitokeza kwenye shamba wakati zao Linaanza kukomaa wao hutafuna dengu kamili hivyo unaweza jikuta unapata hasara wakati dengu zilisitawi vyema, Utatuzi wa chagamoto hiyo ni kuwatega panya kwa sumu kwa ukanda wa mkoa wa shinyanga serikali hutoa dawa nasi huchaganya na mahidi nakusambaza pembezoni mwa shamba maana panya hutokea kwenye nyasi hivyo watakutana na mahidi nakuyala.
- Chagamoto ya Funza baada ya mmea kutoa maua . mmea ukitoa maua funza hushambulia kwa kasi kama eneo hilo liko na funza tiba ya funza hao nikupulizia dawa unaenda duka la kilimo watakupatia.
- Chagamoto ya uhifadh Hapo kunachagamoto ya kushambuliwa na wadudu ndani ya miezi mitatu ya mwanzo unashauriwa kuhifadhi kwenye magunia nasiyo mifuko ya plastic.
Unashauriwa kutia dawa inaitwa AKTERIA mapema kabisa unapohifadhi kama unahifadhi kwa muda mrefu baada ya miezi mitatu unatia tena Au unaweza hifadhi kwaifuko maalumu ambayo imetiwa dawa kabisa na dani inajuwa kama mfuko wa sukari na upaswa kuifuga kitaalamu kama maeelekezo yalivyo .
HALI YA HEWA NA UDONGO
Ni zao linalohitaji hali ya hewa ya kibaridi kiasi kwani joto kali na ukame sana huathiri mavuno yake, hupunguza wingi wa mavuno. Ni zao linalostahimili ukame, linaweza kukua katika hali ya hewa ya unyevunyevu tu.
Kama utakuwa unamwagilia basi epusha unyevu mwingi ikifikia kipindi cha maua hadi kuvuna. Zao hili linaweza kulimwa katika udongo wa aina tofauti tofauti wenye Ph 6-8. Udongo wenye asidi na base kidogo.
Kwa Tanzania zao hili linaweza kulimwa katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Mwanza, Singida, Morogoro, Shinyanga N.K. Lakini kwa sasa mikoa yaShinyanga na Mwanza ndio wazalishaji wakubwa wa Dengu.
UPANDAJI NA NAFASI
Zao hili huitaji mbegu kiasi cha kilogram15 hadi 40 kutegemea ukubwa wa mbegu husika. Zao hili hupandwa mwishoni mwa msimu wa mvua,unaweza kupanda baada ya kuvuna mazao mengine uliyopanda mapema.
Mbegu za dengu hufukiwa katika kina cha sentimeta 5 hadi 6 ili kufanya mazingira rafiki kwa bacteria wa rhizobia kufanya kazi. Zao hili usipande pamoja na viutunguu na tangawizi. Panda kwa kutumia drilling method- bjia ya vifereji kwa nafasi ya mistari miwili ya sentimeta 15 na sentimeta 30 hadi 50 kwa mstari hadi mstari.
UWEKAJI WA MBOLEA
Mbegu unaweza kuzipanda baada ya kuziongeza Mbolea ya samadi kilogram 25 hadi 50 kwa ekari katika shamba lisilo na rutuba ya kutosha.
PALIZI
Palilia mapema shamba lako.
WADUDU WAHARIBIFU KWA DENGU
Dengu hushambuliwa na Mchwa wakubwa weusi, aphid wa njegere, funza wa vitumba, Inzi wa lucina n.k. wazuie wadudu hawa kwa kupuliza dawa za wadudu zisizo kuwa na kemikali yoyote mara tu uonapo dalili za mashambulizi ya wadudu.
UVUNAJI WA DENGU
Zinavunwa mara tuu pindi vitumba vya chini vibadilikapo rangi kuwa kahawia angavu na vitumba vikiguswa hutoa sauti Mavuno ya dengu kwa heka yanaweza kuwa gunia 6,5,4 Inategemeana na eneo ulilolima linarutuba kiasi ngani na umefata taratibu zote.