Fahamu kuhusu homa ya matumbo ya kuku na namna ya kutibu

Share:
Ugonjwa huu husababishwa na bacteria na huwapata kuku wa umri wote. Mara nyingi ugonjwa huu huambukizwa kutoka kwa kuku wagonjwa kwenda kwa kuku wasio wagonjwa kupitia kwenye mayai , chakula chenye kinyesi cha kuku wenye ugonjwa pia watu iwapo watabeba vimelea na kuja navyo kwenye banda.

Jinsi unavyoambukiza:
- Vyakula vya kuku kutoka sehemu yenye ugonjwa kwenda kusiko na ugonjwa.
- Kuku asiye mgonjwa kula vimelea vya ugonjwa kupitia kinyesi cha kuku mgonjwa kwenye chakula.
-  Mizoga ya kuku yenye ugonjwa ikipelekwa sehem isiyo na ugonjwa.
- Kuku mgonjwa huweza kurithisha vifaranga wake kupitia mayai yaliyotagwa.
- Watu na vyombo vya usafiri wanaweza kuhamisha ugonjwa kutoka sehem hadi sehemu.

Dalili za ugonjwa huu ni;
- Homa Kali
- Kinyesi kuonekana kuganda sehem za nyuma.
-  Kiwango cha utagaji hushuka.
- Manyoya husimama
-  Kuku kudhoofika
- Kukosa hamu ya kula.

Kinga:
Tenganisha vifaranga na kuku wakubwa.Kuku wagonjwa watengwe na kupewa tiba ya antibiotic.Zingatia usafi wa banda na vyombo vya chakula na maji.