FAHAMU KUHUSU UFUGAJI WA SAMAKI

Share:

Ufugaji wa samaki unakua kwa kasi sana hapa nchini tanzania kutokana na kuonekana kua na faida sana. hivyo nimeamua leo nikupe elimu kidogo ambayo itakusaidia wewe mfugaji ambaye ungependa kujikita katika ufugaji huo, hivyo tue pamoja ili kujua mengi.

SIFA ZA ENEO LA KUFUGIA SAMAKI
eneo ambalo linavibali vyote vya umiliki
- eneo ambalo soko lake sio la shida
- eneo linalo fikika kwa urahisi
- maji ya kutosha kwa kipindi chote utakacho fuga
- eneo tulivu na lenye usalama wa kutosha
- eneo ambalo halina mmomonyoko wala historia ya mafuriko

NAMNA YA UTENGENEZAJI WA BWAWA LA SAMAKI
i) bwawa la kuchimba na kujengea 





    • ii) bwawa la kuchimba udongo bila kujengea(earthen pond)
      •                

      • UPANDIZIKAJI WA MBEGU ZA SAMAKI KATIKA BWAWA
      • Kabla vifaranga hawaja safirishwa ni vyema kuwatoa katika bwa kubwa wanalo ishi na kuwaweka katika vibwa vidogo vidogo  kati ya masaa 24 hadi 72 kuendana na umbali wa safari bila kuwapa chakula chochote kile.
        • baada ya kuwasafirisha mfugaji  atakiwi kuviweka kwenye bwa moja kwa moja ila inatakiwa maji yalio tumika katika kuwasafirisha yabadilishane joto na maji ya bwawa ambalo wataenda kuishi. hivyo mfugaji anatakiwa kuliweka kontena ambalo vifaranga wamo ndani ya bwawa ambalo wataishi kwa dakika 30 hadi 35 bila kuwafungulia, baada ya hapo kontena liina mishwe taratibu ili kuwezesha maji ya bwawa na yaliyo kwenye kontena kubadilishana na baadae vifaranga watatoka taratibu,

              • - unatakiwa kusafirisha vifaranga wako mda ambao hali ya hewa inakua sio joto yaan mda wa jion na asubuhi ili kuwezesha vifaranga kuimili misukosuko ya safari na bila kupatwa na joto kali.
                • CHAKULA NA UTUNZAJI WA SAMAKI BWAWANI

                - Samaki hutakiwa kupewa chakula angalau mara 2 kila  siku  unatakiwa kuzingatia mda sahihi wa kuwapa chakula yaan asubuhi saa 3-4 na jion saa 9 
              • - samaki upewa vyakula tofauti kulingana na aina.