NJIA ZA KURUTUBISHA UDONGO
Faida za kutifua udongo kama zifutazao;
* Husaidia mizizi kupenya kwa urahisi ardhini
- Baada ya kutifuliwa, udongo hulainika, na mizizi huweza kupenya na kusambaa kwa urahisi ardhini.
* Hulifanya shamba kuwa safi
- Tunapotifua twayang'oa pia magugu taliyoota shambani. Magugu hayo hufukiwa ardhini.
* Hudumisha umbo la udongo
- Kutifua ni kuubomoa uso wa ardhi. Kutifua ni kuufungulia udongo vilango ili maji na hewa vipenye na kuingia kwa urahisi na ndani zaidi.
- Kutifua huwezesha viini na vijidudu kuishi vema zaidi. Huwa bora na la kupendeza.
* Huchanganya rutuba na udongo.
- Mimea iliyobaki ardhini, pamoja na majani au matawi yaliyokufa huchanganywa na udongo wakati tunapotifua mashamba yetu. Pia baada ya kutandaza samadi, au mbolea ya mchanganyiko, ni lazima kutifua ili kuzichanganya takataka hizo na udongo, zioze na kugeuzwa mboji na virutubbisho