JE, NJIA ZA ASILI ZA KUKABILI WADUDU NA MAGONJWA NI ZIPI?
Wadudu na magonjwa ni sehemu ya mandhari ya mazingira. Katika mandhari haya kuna uwiano kati ya mahasimu na wadudu ambayo ni hali ya kimaumbile katika mfumo wa ikolojia.
Viumbe wajulikanao kama wadudu au vijidudu wanaosababisha magonjwa hutambulika kutokana na madhara wanayoleta kwenye mimea. Iwapo mandhari hayatakuwa na uwiano, basi sehemu moja huweza kuwa na idadi kubwa ya wadudu waharibifu hivyo kusababisha madhara.
Madhumuni ya njia za kiasili ni kujaribu kuweka uwiano katika mazingira. Mfumo huu haukusudii kuangamiza wadudu bali kuwakabili.
Ni bora basi kuchukua tahadhari na kuzuia mimea isishambuliwe ili kudhibiti hasara inayoweza kupatikana iwapo mimea itashambuliwa (sio mazao hafifu bali pia ghaama kubwa ya madawa).
Yafuatayo ni maelezo ya kukabili wadudu na magonjwa:
* Vizingiti
* Mitego- Mtego wa mwangaza, Mtego wa inzi na wadudu wanaoruka
* Kuokota kwa mkono
* Kuzuia kwa njia hai
* Dawa za kiasili
* Ushirikiano wa kijamii
* Udongo wenye rutuba
* Mimea yenye rutuba
* Mimea yenye afya
* Mimea inayoweza kuhimili
* Mzunguko
* Afya boa
* Jinsi ya kulima
* Aina ya udongo
* Kupanda kwa wakati
* Kuambatanisha mimea
* Usimamizi na ukaguzi kila mara.