FAHAMU KUHUSU LIMAO

Share:
Rangi ya tunda lililoiva ni njano hadi njano-kijani. Maji yake ina asidi nyingi na ladha yake ni chungu. Matumizi yake ni katika upishi hasa na tunda haliliwi moja kwa moja kutokana na uchungu mkali. Maji yake hutumiwa kwa ajili ya vinywaji ama kama kiungo pamoja na maji ya matunda mengine au mara nyingi kwa kuongeza sukari na maji.
Limau ina vitamini C nyingi ndani yake na kiasi kidogo kinatosheleza mahitaji ya kibinadamu. Sifa hii ilitambuliwa wakati mabaharia kwenye jahazi walipata ugonjwa wa kiseyeseye uliokuwa balaa kwa safari za kwanza zilizovuka bahari za Atlantiki na Pasifiki wakati wa upanuzi wa Wareno, Wahispania na Waingereza kuanzia karne ya 16. Hapa limau zilitambuliwa kuwa dawa lililozuia ugonjwa huu kutokana kiasi chacke cha vitamini C.

Utangulizi
Mti wa limao ambao daima kijani, cirtrus limon, asili yake ni asia. Maji maji ya tunda la limao hutumiwa kwa mapishi na pia maganda yake hutumika hasa wakati wa kupika na kuoka. Majimaji ya limao ni asilimia 5 asidi sitriki ambayo hulipa limao radha ya uchachu, na ph ya 2 mpaka 3, hii hufanya kujipatia aside ya gharama nafuu kwa ajili ya mafunzo ya kielimu. Kutokana na radha yake ya uchachu, vinywaji vingi na peremende vilivyokolezwa na radha ya limao vinapatikana.

 Historia
Asili kabisa ya limao bado haijulikani, japo inaaminika kuwa mimea ya kwanza ilipatikana huko India, Kaskazini mwa Bama na China . Huko Kusini na kusini Mwashariki mwa asia yalifahamika kwa uwezo wake wa matibabu na ukatumika sana kama dawa kwa sumu mbalimbali. Baadae ukafahamika huko Persie na kasha Misri na Iraki mnamo 700bk. Mlimao ulisambaa sana miongoni mwa jamii ya Uarabu na Ukanda wa Mediteraniani kati ya 1000 na 1150 BK. Malimao yaliingia ulaya baada ya karne ya kwanza BK, wakati wa utawala wa Roma.
kilimo cha limao kilianza karne ya kumi na tano huko Genoa. Baadaye kufika mpaka America mwaka 1493 wakati ambapo Cliristopher Columbus alichukua mbegu za limao na kwenda nazo Hispania wakati wa safari zake. Kutoka Hispania malimao yalisambaa sana na yalikuwa yakitumika hasa kwa mapambo na dawa na miaka ya 1700 na 1800, malimao yalikuzwa sana huko Fhorida na Calfonia baada ya malimao kuanza kutumika kupikia na kama viungo vya kuongeza laza. Mnamo 1747 utafiti wa James Lind ulithibitisha kwamba tunda la limao lina vitamini C na yaliweza kuwatibu baharia ugonjwa wa ngozi wa kiseyeye.
Virutubisho vya limao
Malimao yanafahamika kama msaada mkubwa wa umengenywaji wa chakula, mchanganyiko wa asali nyeusi na makapi huwa kwa kiwango kizuri katika kusafisha oganiza umegaji wa chakula. Virutubisho vingine hujumuisha maji -89%, aside ya sitriki -5%, makapi -2.8%, sukari – 2.5%, mafuta – pungufu ya 0.3%, protini – pungufuya 7%, vitamin C, na madini kadhaa kama vile selenium, zinc manganese, na shaba. Vitamin C. kula limao lililokomaa huwezesha mtu kupata 10,000% ya vitamin c. Zingatia kuwa ni lile ganda la ndani jeupe la ndani la limao, linalokuwa na kiasi kikubwa cha vitamin c kwa ujazo wake kuliko chakula kingine chochote, uchunguzi unaonyesha, sehem ile nyeupe kuwa na mara 8 mpaka 11 zaidi ya vitamin c kuliko chupa ya dawa ya vitamin c kutoka hospitali.