SIFA ZA BANDA BORA LA KUKU
Liwe na kuta, paa na sakafu imara. kuta na sakafu zisiwe na nyufa Liwe na sehemu ya kuku kutagia, kuatamia na sehemu ya kulea vifaranga. Liwe na vichanja kwa ajili ya kuku kupumzika na kulala. Liwe na nafasi ya kutosha kulingana na idadi ya kuku Liwe na uwezo wa kuingiza mwanga na hewa ya kutosha. Liwe na nafasi inayoruhusu mtu kuingia na kufanya usafi.
SEHEMU INAYOFAA KUJENGA BANDA LA KUKU.
Isiyokuwa na mteremko mkali. Isiyoruhusu maji kutuama. Iwe sehemu inayoruhusu hewa na mwanga wa kutosha. Ikiwezekana iwe sehemu yenye kivuli.

AINA ZA MABANDA YA KUKU.
Uchaguzi wa aina ya banda la kuku hutegemea mazingira. Kuku wanaofugwa kwenye mazingira ya joto wanahitaji banda lenye ukuta mfupi na sehemu kubwa ya uwazi wenye wavu hadi kufikia kwenye paa kulinganisha na sehemu zenye baridi ambapo,banda linahitaji kuwa na ukuta mrefu unaokaribia paa na sehemu ndogo tu,iliyo na uwazi wenye wavu ili kupitisha hewa na mwanga.vilevile eneo lenye matatizo kama ya majimaji au wanyama wanaoshambulia kuku inabidi kujenga aina ya banda lenye sakafu iliyonyanyuliwa juu.

VIFAA VINAVYOTAKIWA KATIKA UJENZI WA BANDA.
Vifaa vya kujengea banda vizingatie gharama na upatikanaji wake katika eneo husika.Vifaa hivyo vimepangwa katika makundi yafuatayo:

- Vifaa vya kujengea sakafu Sakafu la banda la kuku linaweza kujengwa kwa kutumia,saruji,udongo,mbao, mianzi au fito.
- Vifaa vya kujengea kuta kuta zinaweza kujengwa kwa kutumia , fito,udongo,matofali,mawe, mabati,mianzi,wavu,mabanzi au mbao.
- Vifaa vya kujengea paa. Paa la banda la kuku linaweza kuezekwa kwa kutumia nyasi, makuti, bati, migomba na vigae kulingana na uwezo wako.
- Vifaa vya kujengea wigo Wigo unaweza kujengwa kwa kutumia mbao,mianzi,matete,wavu, matofali,miti, au fito,mabanzi au mabati.
UKUBWA WA BANDA LA KUKU KULINGANA NA IDADI YA KUKU
Ukubwa wa banda la kuku unategemea na idadi ya kuku na aina ya kundi la kuku.Kuku wanaweza kugawanywa katika makundi mbalimbali kutegemea umri wao na madhumuni ya uzalishaji.