Kutifua ni kuupindua udongo lakini, kwa kweli jembe la mkono haliwezi kuupindua udongo vema. Ukitaka kuitifua ardhi yako kwa makini kwa kulitumia jembe lako la mkono, fanya kionyeshavyo kkielezo, hasa kama ardhi ina magugu, takataka au nyasi au mimea inayoufunika udongo.
Kwanza lima mtaro au mfereji. Kisha pitisha jembe lako juu juu tu kuondoa tabaka la juu pamoja na mimea au takataka zilizopo hapo (1)
Livute jembe kwako na kuvuta udongo ule wa juu na takataka zote ziingie kwenye mtaro au mfereji huo.
Kisha piga jembe kwa nguvu uivunje ardhi iliyo chini ya tabaka ile. Livute jembe kwako pamoja na udongo wake.
Udongo huu utayafunika yaliyomo kwenye mtaro (2) (1), (2) Tazama kielelezo ukurasa ufuatao
Magugu yote na takataka au majani yaliyoota hufukiwa kwenye mtaro na kufunikwa.
Kule yataoza.
Shamba lako litabakia kuwa safi siku nyingi.
Shamba lako litakuwa na mboji kwa wingi.
Kutifua kwa beleshi au kwa chombo kama uma
Kuna baadhi ya vifaa vingine vinavyotumika kwa kutifua udongo. Beleshi hutumika zaidi katika kilimo cha mboga ikiwa sehemu ya bustani ina mboji kwa wingi.
Chuma cha beleshi
Kimenyooka moja kwa moja na mpini wake. Unapotifua kwa beleshi ni kama kutumia jembe ila utatumia mguu wako kwa kukisukuma chuma cha beleshi kwenye udongo na kukata bonge la udongo.
Hakikisha udongo unafukia nyasi na takataka vizuri
Kuna baadhi ya vifaa vingine vinavyotumika kwa kutia udongo. Beleshi hutumika zaidi katika kilimo cha mboga ikiwa sehemu ya bustani ina mboji kwa wingi.
Chumba cha beleshi
Kimenyooka moja kwa moja na mpini wake.
Unapotifua kwa beleshi ni kama kutumia jembe ila utatumia mguu wako kwa kukisukuma chuma cha beleshi kwenye udongo na kukata bonge la udongo
Hakikisha udongo unafukia nyasi na takataka vizuri.
Ukilima kwa njia hii hutakanyaga kwenye udongo uliolimwa. Hivyo udongo hautakuwa mgumu. Aina nyingine za mboga huhitaji kilimo cha namna hii.