Fahamu zaidi kuhusu ugonjwa wa Gumboro ( Infectious Bursal Diseases) unaowasumbua wafugaji wa kuku.

Share:

Ni ugonjwa wa  utokanao na virusi  viitwavyo ”BIRNAVIRUS" . Ugonjwa huu huwashambulia kuku na ndege wengine wafugwao. 
i.Kuenea/kusambaa kwa ugonjwa.
ii.Kutoka banda moja kwenda linginge.
iii.Kupitia kinyesi kinyesi cha kuku anayeumwa.

Dalili za Ugonjwa
Kuku hutapika na kuharisha majimaji.

Manyoya husimama.

Kuku husinzia na kukosa hamu ya kula.

Vifo hufikia hadi asilimia thelathini (30%).

Kuku hujidokoadokoa sehemu ya haja kubwa.

Cloaca huvimba.

Chini ya ngozi hasa mapajani vidonda hutokea hasa vifaranga.

Namna ya kukinga na kuzuia ugonjwa wa Gumboro
Safisha banda kwa dawa za kuua vijidudu (Disinfectants).

Wapatie chanjo ya Gumboro vifaranga wakiwa na umri wa wiki 2 na rudia tena wakiwa na umri wa wiki 3 (yaan siku ya 14 na 21)

Tiba za ugonjwa wa Gumboro
Hakuna matibabu ya ugonjwa huu, ila kwa msaada zaidi wasiliana na mtaalam au daktari wa mifugo. Asante