Kulima kwa kuchanganya mazao:
Mazao ya nafaka kama mahindi au mtama hustawi vizuri pamoja na jamii ya kunde yaani maharage, karanga, choroko, kunde kwa sababu zao la jamii ya kunde hurutubisha udongo.
MSETO WA MAZAO NA MITI
Huu ni mtindo wa kilimo ambamo miti mikubwa na midogo huingizwa katika mfumo mmoja na mazao, na hivyo kuoteshwa katika shamba moja. Miti hupandikizwa ama pembezoni mwa shamba ii kuonyesha mipaka, au ndani ya shamba kwa nafasi maalum, au ndani ya shamba kwa nafasi maalum, au ndani ya shamba kwa nafasi maalum, au hupandikizwa katika kanda mbalimbali ili kuleta kivui kwa baadhi ya mazao.
FAIDA YA MTINDO HUU WA KULIMA NI :-
i. Baadhi ya miti kama lukina hurutubisha udongo kutokana na naitrojeni inayotengenezwa katika mizizi yake.
ii. Migunga, Mikwaju na Kavilea hurutubisha udongo kutokana na majani yake yanapodondoka na kuoza chini yake. Kutokana na rutuba hii mazao mbalimbali huweza kustawi vizuri chini ya miti hii.
iii. Pia husaidia kudhibiti mmomonyoko wa udongo
Angalia:
Mbolea za chumvichumvi au Mbolea za viwandani zinazouzwa kwenye maduka ya kilimo haziongezi rutuba shambani. Lakini zimejaa chumvichumvi.
Chumvichumvi hizi haziupi udongo umbo la kupendeza kwa kuwa hazina mboji. Huziwezi kulingana na samadi au mbolea ya mchanganyiko, au kupumzisha ardhi
* Kupumzisha shamba, Kutandaza mabua, nyasi na majani, Kutandaza samadi, mbolea ya mchanganyiko na udongo wa zizini, Kutumia mbolea ya kijani, Kilimo cha mzunguko wa mazao
*Kilimo cha mseto wa mazao, au mseto wa mazao na miti: Mbinu hizo zote huuongezea udongo rutuba halisi. Hulifanya umbo la udongo kupendeza zaidi, hivyo maji na hewa hupenya ndani vema, na mizizi husambaa kwa urahisi na kukua vema.